Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Wednesday, March 24, 2010

Dr Ufuta enzi hizo na sasaJohn,

Mimi ni mmjoja kati wa fans wa blog yako. Nilikuwa Morogoro mjini na kwa bahati nzuri wakati napata chai ya jioni pale B1 restaurant akapita mwanamuziki mkongwe DOKTA UFUTA Nilifanya nae maongezi mafupi maana alikuwa na haraka kidogo akiwahi kazini, kwa sasa ni mlinzi wa usiku" babu mlinzi" katika moja ya makampuni ya ulinzi pale Morogoro. Tuliongea sana na nikakumbuka last article uliyotoa ya Cuban Marimba na jinsi alivyokuwa akionenaka kijana very hundsome. sasa kupitia taswira hizi chache hivi ndivyo alivyo.

Louie
(Dr Ufuta ndiye mwenye miwani katika hili ganda la santuri enzi hizo)

10 comments:

John F Kitime said...

Kaka John, kwanza kabisa nakupungeza kwa kazi nzuri unayoifanya. nimefurahishwa sana na uwepo wa blog hii inatakayotupatia mambo mbalimbali kuhusu muziki wa Kibongo. Kitu kizuri zaidi katika blog yako siyo kwamba inatupa habari, ni kwamba inatoa pia elimu na kutupa tafakari juu ya masuala mbalimbali katika anga ya Muziki. zaidi ya hapo kwa wanamuziki wa sasa inawapata kwelekeo juu ya future zao. Mimi niko pamoja na wewe na nitakuwa nikipa Updates kila nitakapokuwa nikikutana na suala la kimuziki huko ninakozunguukia.

--
Hassan Bumbuli
Senior Editor
Si Mchezo! Magazine
P.O.Box 2065
Patel Building 5th Flour Opp Kazi House
+255 713 436153
Dar es Salaam

Mzee wa Changamoto said...

Haya maelezo yana nguvu za ajabu.
Tumkumbuke huyu na wengine wengi WALIOITUMIKIA NCHI NA SASA WAMETELEKEZWA.
Mkumbuke Mzee Nyunyusa na ngoma zake, na wengine waliosaidia kusambaza na kutekeleza sera na mipango ya serikali kama GEZAULOLE ama hata walioitumikia jamii kwa kufunza mengi kupitia tunzo zao. Lakini sasa hivi wako wapi ama heshima, stahiki na haki zao ziko wapi?
Niliwahi kuandika kuhusu wasanii katika toleo nililolipa kichwa cha habari WASANII KAMA CHOMBO CHA STAREHE CHA SERIKALI (http://changamotoyetu.blogspot.com/2008/10/wasanii-kama-chombo-cha-starehe-cha.html) na baadae nilikuja kujiuliza na kushiriki kuuliza kuwa NI LINI TUTAKAPOWAENZI WATU HAWA? (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/08/ni-lini-tutawaenzi-watu-hawa.html).

Naamini kuna funzo la msingi katika picha na bandiko hili.
TUJIFUNZE

John F Kitime said...

kWA WALE AMBAO TUMESHATUMIKA HIVYO MARA MIA KIDOGO TUNAIJUA FRUSTRATION YAKE. Kwanza aslimia kubwa ya viongozi hufanya diplomasia ya kuonyesha meno tu lakini hawana interest yoyote ya wasanii na usanii wao, hivyo ni protokali tu inayowafanya wavumilie. Na ingekuwa wanajali wangekuwa japo wanajiuliza hawa jamaa wako hapa wamelipwa? Bahati mbaya kwa hili hakuna tofauti kati chama tawala na vile vinavyotaka kutawala

SIMON KITURURU said...

Inasikitisha!

Baraka Mfunguo said...

Ni changamoto katika maisha ya wanamuziki Tanzania juu ya nini kifanyike na pia kuwathamini na kuwaenzi wale wakongwe wa Muziki Tanzania naamini wapo wengi tu sasa hivi wamekwishasahaulika. Kitu kilichofanya hawa wakongwe wetu kuwa maskini mpaka leo hii naweza kusema ni utii waliokuwa nao juu ya sera za nchi yetu miaka hiyo maskini kumbe hawakujua kwamba haki zao zinaliwa.

Naweza kusema hawa walikuwa wanamuziki wa ukweli kutokana na tungo zao, ujumbe wao na namna yao ya kuonekana jukwaani na nje ya jukwaa iliendana na mahadhi ya utamaduni wa kwetu Tanzania.

Anonymous said...

Tunzo za mwaka huu ambazo zinafanyika kwa mwaka wa 11 sasa zimepangwa kutolewa kwenye Ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam, Mei 14.

Wanaowania tuzo ya Mwimbaji bora wa kike.Lady Jaydee
Mwasiti Almasi
Maunda Zorro
Vumilia Mwaipopo
Khadija Yusuph
wanaowania tunzo ya Mwimbaji bora wa kiume.
Marlow
Banana Zorro
Mzee Yusuph
Alikiba
Christian Bella


Wanaowania Albamu Bora ya TaarabJahazi Modern Taarab (Daktari wa Mapenzi),
5 Stars Modern Taarab (Riziki Mwanzo wa Chuki),
Coast Modern Taarab (Kukupenda Isiwe Tabu),
New Zanzibar Star (Powa Mpenzi)
East African Melody (Kila Mtu Kivyakevyake).Tunzo ya Wimbo Bora wa Taarab inawaniwa na


Daktari wa Mapenzi’ na ‘Roho Mbaya Haijengi’ (zote Jahazi Modern Taarab), ‘Wapambe Msitujadili’, ‘Riziki Mwanzo wa Chuki’ (zote 5 Stars Modern Taarab) na ‘Kukupenda Isiwe Tabu’ (Coast Modern Taarab).

Tunzo ya Wimbo Bora wa Mwaka inawaniwa na


Marlow ‘Pii Pii-Missing my Baby
Diamond (Kamwambie)
Banana Zorro (Zoba)
Hussein Machozi (Kwa Ajili Yako).Tunzo ya Wimbo Bora wa Kiswahili kwa upande wa bendi ni


Machozi Band (Nilizama),
African Stars Band-Twanga Pepeta (Mwana Dar es Salaam),
Top Band (Asha),
FM Academia (Vuta Nikuvute)
Extra Bongo (Mjini Mipango).Tunzo ya Albamu Bora ya Bendi inawaniwa na


African Stars Band ‘Twanga Pepeta’ (Mwana Dar es Salaam),
Kalunde Band (Hilda)
Msondo Ngoma Music Band (Huna Shukrani).

Kwa upande wa Tunzo ya Wimbo Bora wa R&B, wanaoiwania ni


Belle 9 ‘Masogange’,
Diamond (Kamwambie),
AT na Stara Thomas (Nipigie),
Maunda Zorro (Mapenzi ya Wawili)
Steve (Sogea Karibu).Tunzo ya Wimbo Bora wa Asili ya Kitanzania unawaniwa na


Mrisho Mpoto (Nikipata Nauli),
Machozi Band (Mtarimbo),
Offside Trick (Samaki),
Wahapahapa Band (Chei Chei)
Omari Omari (Kupata Majaaliwa).Wanaowania Tunzo ya Wimbo Bora wa Hip Hop ni


Joh Makini (Stimu Zimelipiwa),
Quick Racka (Bullet),
Chid Benzi (Pom Pom Pisha),
Mangwea (CNN) na Fid Q (Iam a Professional).
Tunzo ya Wimbo Bora wa Reggae inawaniwa na


Hemedi (Alcohol),
Dabo Ft. Mwasiti (Don’t Let Go),
Man Snepa (Barua)
Matonya Ft. Christian Bella (Umoja ni Nguvu).
Kwa upande wa Tunzo ya Wimbo Bora wa Ragga, wanaoiwania niDully Sykes (Shikide),
Bwana Misosi (Mungu yuko Bize),
Drezzy Chief (Wasanii)
Benjamin wa Mambo Jambo (Fly)Tunzo ya Rappa Bora wa Mwaka inawaniwa naChokoraa,
Ferguson,
Kitokololo,
Totoo ze Bingwa
Diouf.Tunzo ya Msanii Bora wa Hip Hop ni
Joh Makini
Fid Q
Chid Benz
Mangwea
Profesa Jay.Tunzo ya Wimbo Bora wa Afrika Mashariki inawaniwa na


Blue 3 Ft. Radio and Weasal -Good Life ‘Where you are’,
Kidumu Ft. Juliana (Haturudi Nyuma),
Cindy (Na Wewe),
Radio and Weasal - Good Life (Bread and Butter)
Kidumu akitupa karata na wimbo ‘Umenikosea’.
Tunzo ya Mtunzi Bora wa Nyimbo niMzee Yusuph
Mrisho Mpoto
Lady Laydee
Banana Zorro
Mzee Abuu, Fid Q


Tunzo ya Watayarishaji Bora wa Muziki

Lamar
Marco Chali
Hermy B
Allan Mapig0
Man Water


Video Bora ya Muziki wa Mwaka inawaniwa na


Lady Jaydee (Natamani kuwa Malaika)
Diamond (Kamwambie),
AY (Leo)
Banana Zorro (Zoba)
C Pwaa (Problem).Tunzo ya Wimbo Bora wa Afro Pop inawaniwa na


Banana Zorro (Zoba)
Alikiba (Msiniseme)
Marlow (Pii Pii Missing My Baby)
Mataluma (Mama Mubaya)
Chegge (Karibuni Kiumeni)
Tunzo ya Msanii Bora Anayechipukia


Belle 9
Diamond
Barnaba
Quick Racka
Amini


Tunzo ya Wimbo Bora wa Kushirikiana inawaniwa na


AT - Stara Thomas (Nipigie)
Mangwea Ft. Fid Q (CNN)
Barnabas Ft. Pipi (Njia Panda)
Mwana FA Ft. Profesa Jay na Sugu (Nazeeka Sasa)
Hussein Machozi Ft. Joh Makini (Utaipenda).

Danstan said...

Bwana Kitime,

Niko katika suala hili hili la wanamuziki wa zamani, kuishia katika maisha duni au kufanikiwa....niulize, je, unamfahamu mwanamuziki wa Kongo, Boni Efokoko aliyewahi kuwa na bendi mbali mbali hapo Tz? Aliwahi kupiga bendi gani na alikuwa akishiriki katika ala ipi?

Danstan

Anonymous said...

Jamani niliomba msaada wa hiyo player hapo pembeni, lakini comment yangu haikutolewa imekuwaje? Maana nikitaka ku play inaruka wimbo mmoja kwenda mwingine bila kuimba chochote! Bw. Kitime nisaidie!

JFK said...

Mkuu ngoja nijaribu kubadilisha settings tuone kama itasaidia, samahani kwa kukosa raha

Anonymous said...

Mzee Kitime tunashukuru sana kwa kazi yako ya kutuhabarisha na kutukumbusha mambo ya muziki hasa ule wa zamani.
Nina swali moja kuhusu majina ya utani ya wasani (vijana wa siku hizi hupenda kutumia neno aka). Kwa mfano Dr Ufuta na Dr Remmy. Nini hasa kiini cha wanamuziki hawa kuitwa (kujiita) Dr. Inawezekana ni kwa sababu ya umahiri wao ktk fani au chombo walichokuwa wakipiga katika bendi zao?
Zamani kulikuwa na matangazo ktk magazeti yakionyesha bendi gani inapiga wapi. Ktk matangazo haya, nakumbuka vizuri kuona Dr Remmy Ongala akiwa amejipamba kwa vitu vya asili kama vile hirizi, vibuyu (sina uhakika kama ni neno la kiswahili au kingoni). Je inawezekana hii ilichangia kwa Remmy kupewa U-Dr, hasa akifananishwa na waganga wa jadi?
Kuna bendi moja aliibuka kipindi fulani, iliikuwa inaitwa The Mk Beats (wana Tukunyema mpaka chini) ikiongozwa mtu mzima Shem Kalenga. Nafikiri huyu mzee amesahaulika kidogo, kama unaweza kutupa historia yake fupi tutafurahi.
Nakumbuka wimbo wake mmoja ulikuwa unaimbwa .. ndela ombwe x2.. (sina uhakika kama nimepatia. Ulikuwa ukianza kwa horn ya treni na mwimbaji akisema Kigoma, Tabora, Jijini DSM.
Shukrani mkuu

Adbox