YOUTUBE PLAYLIST

Saturday, March 13, 2010

The Comets


Hawa ni wanamuziki wa The Comets kabla hawajawa the Sparks. Haya wadau nani unamfahamu hapa? Una stories za wakati huo. Nilipata bahati ya kuwasikia 1969 pale ambapo iko shule ya Forodhani wakipiga bugy, na ilikuwa mara yangu ya kwanza kusikia wimbo Mammy Blue, haujanitoka kichwani mpaka leo. Nakumbuka pamoja na nyimbo kama Direct Me, Hard to Handle, walipiga nyimbo za Isaac Hayes (Black Moses) ambazo zilikuwa top kwa wakati huo, unaukumbuka Move on?

6 comments:

  1. Anonymous00:39

    Mkuu,

    Documentation ni muhimu sana. Kama tungekuwa na mtindo wa kuweka matukio kwa maandiko kwenye hiyo picha tungewajua wote.

    Samahani, hivi Adam Kingui aliishia wapi? Na huyo Dada kwenye picha siyo yule Msouth Africa Judith Hadebe? Wazazi wake walikuwa wanaishi mitaa ya Ilala Shariff Shamba karibu na kwa kina Sabuni? Mungu atusamehe Judith Hadebe mara ya mwisho nilimuona akiwa anamiliki baa ikiitwa Lady Madonna mitaa ya Mikocheni inayopakana na kituo cha Satelite Mwenge.

    ReplyDelete
  2. Naomba Mungu kuwa hii blog ituamshe kuhusu issue ya kudocument mambo, maana hata blogs za wanamuziki wetu wa sasa ni kama za kufanya promo kwa ajili ya kazi fulani, japo nayo ni afadhali kuliko kukosa kabisa lakini tunahitaji taratibu za kudocument vitu vyetu kitaalamu zaidi. Wasomi wetu wanadeni katika hili hawajaitendea haki nchi yao maana asilimia kubwa ya vitabu au maandiko utakavyopata reference ya mambo mengi ya nchi hii yameandikwa na wageni, tatizo ni kuwa wengine au wamepewa habari si za kweli au wana ajenda ya siri hivyo kupindisha ukweli, kwa hiyo ni tatizo kubwa. Nasoma maandiko ya Mmarekani mmoja ambaye najua alikaa sana Tanzania, anadai Watanzania wanapenda sana kipindi cha zilipendwa kwa kuwa hupiga nyimbo za kusifu ujamaa, kwa hiyo wanakumbuka wakati ambapo mambo yalikuwa mazuri. Na huyu ni Associate proffessor wa Chuo kimoja USA, na anaitwa mtaalamu wa muziki wa Tanzania, ni wazi ana ajenda yake iliyojificha kuhusu maandiko haya.

    ReplyDelete
  3. Anonymous12:08

    John,
    umeanzisha blog ambayo inatakiwa kuungwa mkono na wadau wote. Kwangu nina kazi ya kutafuta kumbukumbu ambayo naweza kuipost na kuwakumbushia wale wa umri huo,moja ya magazeti yenye picha na taarifa nzuri liikua ni pamoja na gazeti la TAIFA la Kenya

    ReplyDelete
  4. Anonymous14:59

    Ndg John,
    Kwamara ya kwanza nimeingia kwenye blog yako baada ya kupata taarifa zake kwa mmoja kati ya wasanii wachache wa muziki wa asili Dr. Zawose Jr. Nimefurahi sana kwa kila kilichoandikwa huko na pia mawazo ya wachangiaji wote , japo najua wapo wachache sana wanaweza kuwa wanapotoka ama kupotosha jamii kwa maoni yao.

    Nikweli kwamba wasomi wetu wana deni kubwa sana katika ulimwengu wa kutunza kumbukumbu maana tafiti nyingi zilizofanywa na wasomi wazalendo, wao wenyewe hawazithamini na wanazirusha kwenye maeneo ambapo hazitaweza kupatika ka urahizi.
    Huyo msomi wa USA uliye tueleza habari zake hebu tupe detail tumpatie changamoto za kweli na halisi ili hata hawo wanasoma chapishi zake waweze kumuona kwa jicho la tatu. nakutakia kheri katika kila lalkheri katika ziara zako huko USA

    ReplyDelete
  5. Patrick Tsere17:51

    Kwenye hiyo picha ya The Comets aliyekaa kwenye spika ni Michael Mhuto na kitini akipiga rythm ni marehemu Lameck Ubwe wakati huo akiwa form 3 Agakhan (hivi sasa Tambaza). Comets iliundwa baada ya Hot 5 ya akina Michael na Green Jackson kusambaratika na wao kuanzisha Tonics na Sweetie Francis, Adamu Salum aka Addy Sally. If my memory serves me right

    ReplyDelete
  6. Patrick Tsere17:58

    Adam Kingui alishafariki miaka mingi iliyopita.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...