Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Monday, March 1, 2010

Chinyama Chiyaza

Tangazo jingine la dansi la miaka hiyo ambalo nina uhakika litaleta kumbukumbu kwa wapenzi wa Maquis wa enzi hizo za Mtindo wa Telemka Chekecha Scania LBT III, wakati huo gari za Scania ndizo zilikuwa maarufu nchini na Scania LBT III ilikuwa gari yenye saiz kubwa kuliko zote, na ndio yenye kusifika zaidi, karibuni tena wapenzi wa White House mchangie, mambo yalikuwa mazito chini ya uongozi wa Chinyama Chiyaza ambae alikuwa mpiga Saxophone katika bendi. Wakati huu Maquis ilikuwa na maendeleo makubwa sana ya kuwa na mashamba, magari, matrekta na hata kuwa na Kota zake pale Sinza Palestina. Hebu angalia majina yaliyopo katika bendi.

4 comments:

Anonymous said...

Mkuu,

Hiyo link hapo chini inaweza ongeza utamu wa mada hii

http://www.arushatimes.co.tz/2004/27/interview.htm

John F Kitime said...

Aksante anon kwa kutuongezea utamu hapa

Anonymous said...

Kitime!
Hii blog sii ya mchezo. Huko nyumbani kwa wale wanaoujua "muziki' wa nyakati zetu, bila ya shaka wanakila haki ya kujivunia uwepo wa Blog hii ya watu makini.
Huyo anon amelenga maana baada ya kusoma mambo kwenye hiyo link nimekumbuka mbali sana. Vipi mnakuja lini London? tunawangoja kwa hamu sana tupate zenu tungo mpya. nasikia siku hizo mko juu.
Kila la kheri John.

Anonymous said...

Mkuu, shukurani kwa kutukumbusha mambo ya kina Chinyama Chiyaza wa Marguiz du Zaire. Marekebisho kidogo tu kwenye post yako, nadhani mtindo wao ulikuwa scania LBT 111 na si FBT.
Endelea kutuletee habari za vijana wa zamani.

Adbox