Posts

Showing posts from March, 2010

Miaka minne toka kifo cha Moshi WIlliam

Image
Tunakukumbuka Moshi. Mola akulaze pema peponi
Image
Unamkumbuka msanii huyu?
Image
Katika makala za hapo nyuma tulitaja kundi la Barlocks lililokuwa na makao yao pale juu ya Patel Stores , jengo linaloangaliana na Printpak, Barlocks lilikuja badilika na kuwa Mionzi. Kundi hili la Mionzi lilikuwa likipiga mara nyingi New Afica Hotel katika ukumbi wa Bandari Grill na Kilimanjaro Hotel pale Simba Grill. Habari zaidi kuhusu kundi hili zinafuata lakini hapa kuna picha ya kundi hili wakati huo akiwemo Innocent Galinoma, Martin Ubwe, na Frank

Dr Ufuta enzi hizo na sasa

Image
John,

Mimi ni mmjoja kati wa fans wa blog yako. Nilikuwa Morogoro mjini na kwa bahati nzuri wakati napata chai ya jioni pale B1 restaurant akapita mwanamuziki mkongwe DOKTA UFUTA Nilifanya nae maongezi mafupi maana alikuwa na haraka kidogo akiwahi kazini, kwa sasa ni mlinzi wa usiku" babu mlinzi" katika moja ya makampuni ya ulinzi pale Morogoro. Tuliongea sana na nikakumbuka last article uliyotoa ya Cuban Marimba na jinsi alivyokuwa akionenaka kijana very hundsome. sasa kupitia taswira hizi chache hivi ndivyo alivyo.

Louie
(Dr Ufuta ndiye mwenye miwani katika hili ganda la santuri enzi hizo)

Bendi za Wilayani nje ya Dar Es Salaam

Image
Nimeona nirudie tena posting hii pengine iliwahii mno, miaka iliyopita karibu kila wilaya ilikuwa na bendi, naomba tusaidiane kukusanya kumbukumbu hizi muhimu kwa historia ya muziki wa Taifa letu. Kwa mfano pale Same niliwahi kukuta band ya Tanu Youth League siikumbuki jina lake, pia nimeshakuta bendi pale Igunga, Mwadui, Sumbawanga, Makambako, kule Mbeya, nakumbuka ilikuweko bendi ya Bwana Remmy, hebu tuchangie tuone tutafika wapi. Bendi hizi ziliwahi kutoa vibao vingi vilivyotingisha anga za muziki wakati huo. Kwa mfano Shinyanga Jazz na kibao chao Tenda wema uende zako kilichotungwa na kuimbwa pia na Mzee Zacharia Daniel, ambae mpaka kifo chake aliitwa Mzee Tenda wema, au vibao vya Mzee Zahir Ally Zorro akiwa na Kimulimuli, Kabwe,Tausi na vingi vingine , waliopitia JKT Mafinga wakati huo wanakumbuka raha ya bendi hii. Unajua kwanini Bendi iliitwa Kimulimuli? Bendi ilipata taa za stage zinazowakawaka zilizokuwepo pamoja na bendi kwa hiyo taa hizo kumulikamulika ndo kukatoa jina la K…

Cuban Marimba

Image
Kuanzia miaka ya1920 mpaka 1940 Tanzania, hususani Tanzania bara, wanamuziki na wapenzi wa muziki walifuatilia sana muziki kutoka Cuba kupitia sahani za santuri za wakati huo. Kulikuwa na vikundi kama Trio Matamoros and Sexteto Habanero, ambao walitoa santuri zikiwa na namba zinazoanzia GV1, GV2na kuendelea na kupata upenzi mkubwa katika ukanda huu wa Afrika. Ni vikundi hivi ambavyo viliingiza mitindo kama rhumba, Bolelo, Chacha na kadhalika. Kwa kweli bendi za muziki wa dansi zingepata mengi ya kimapinduzi kama zingeweza kusikiliza na kuelewa muziki wanaoupiga kiini chake ni nini.Kutokana na hamu hiyo ya kuujua na kuupiga muziki wa kicuba kisawasawa Marehemu Salum Abdallah aliwahi kutoroka kwao Morogoro akakimbilia Mombasa ili apande meli aende Cuba, bahati mbaya safari yake iliishia Mombasa kwa kuishiwa fedha, ambako alianza kupata shida lakini kwa kuwa baba yake alikuwa mwarabu, Ushirika wa waarabu wa Mombasa walimtaarifu mzee huyo kuhusu alipo mwanae na alimfuata na kumrudisha Mor…

Mheshimiwa mchango wako ni muhimu

Nimekuwa najaribu kumshawishi Mheshimiwa mmoja ambaye alikuwa Waziri kwa muda mrefu na sasa ni Mbunge atoe mchango katika blog hii, Mheshimiwa huyo katika miaka ya sitini alirekodi nyimbo moja nzuri sana ya kumsifu Mwalimu Nyerere. Mheshimiwa huyo alirekodi kibao hicho wakati akisoma Uholanzi.
Pia Balozi mmoja maarufu aliyekuwa akiimba nyimbo za James Brown miaka hiyo najaribu kumwomba ruksa atusaidie experience zake.
Mzee moja marehemu sasa lakini ana watoto wengi wanamuziki, japo yeye alikuwa mwalimu Tabora school alinieleza kisa cha Mheshimiwa mmoja (Mbunge muhimu), ambaye nitamwomba ruksa yake nitaje jina lake baadae, ambaye alilazimika kuwa anamlimia kajibustani kake ili afundishwe gitaa. Nashukuru kuwa mheshmiwa huyo mpaka sasa ni msaada mkubwa sana katika fani ya muziki hasa wa dini

LIBENEKE

Mheshimiwa mmoja kaniomba niweke mwanga kwenye hili neno ambalo limetajwa hapo juu. Katika kumbukumbu zangu, Libeneke ulikuwa mtindo wa Butiama Jazz Band, bendi iliyokuwa chini ya uongozi wa marehemu mzee Mkwega, ikiwa na mpiga solo mzee Makelo ambae yuko Shikamoo Jazz, baadhi ya waimbaji akiwemo Saidi Hamisi ambaye kwa miaka mingi mpaka kifo chake alikuwa Vijana Jazz. Kulikuweko na wimbo ambao ulikuwa maarufu ukiwataja wanamuziki wa bendi hiyo na kibwagizo chake kilikuwa ....waache waseme, watachoka wao mtindo libeneke utatia fora...... Mkuu wa libeneke upo? Karibu wapenzi wa Butiama Jazz

The Tanzanites

Image
Kabla ya kuwa na jina hili waliitwa the Barkeys, moja ya bendi za zamani sana Tanzania picha hii ya siku ya mwaka mpya 1991 itawapa watu kumbukumbu za kutosha. Bibie hapo mbele ni Juliet Seganga

Wanamuziki ndugu 1

Image
Katika historia ya muziki kumekuweko na familia kadhaa ambazo zimekuwa zikitoa wanamuziki zaidi ya mmoja. Moja ya familia iliyokuwa maarufu ilikuwa ni familia ya akina Sabuni. Unawakumbuka? Niko katika mawasiliano na mwanamuziki mmoja aliyepiga na ndugu watatu kati ya hao na tutapata kumbukumbu nyingi karibuni

Kushoto Cuthbert Sabuni, chini ni Raphael Sabuni akiwa na mwimbaji wa kike ambaye bado natafuta jina lake lakini alijulikana kama 'Lady Soul'

The Comets

Image
Hawa ni wanamuziki wa The Comets kabla hawajawa the Sparks. Haya wadau nani unamfahamu hapa? Una stories za wakati huo. Nilipata bahati ya kuwasikia 1969 pale ambapo iko shule ya Forodhani wakipiga bugy, na ilikuwa mara yangu ya kwanza kusikia wimbo Mammy Blue, haujanitoka kichwani mpaka leo. Nakumbuka pamoja na nyimbo kama Direct Me, Hard to Handle, walipiga nyimbo za Isaac Hayes (Black Moses) ambazo zilikuwa top kwa wakati huo, unaukumbuka Move on?

Nawaachia wananchi waseme 2

Image

Mitindo ya Bendi Zetu

Kuwa na mitindo au staili ya muziki limekuwa jambo la kawaida kwa bendi zetu hapa Tanzania. Zamani mtindo mpya ulikuwa ni mapigo mapya ya muziki au hata uchezaji mpya. Hata bendi ikiwa mpya ulitegemea iwe na mapigo mapya na hivyo kuwa na maana ya kuwa na mtindo mpya. Hii ilifanya upenzi au unazi wa bendi kama ilivyojulikana wakati huo kuwa mkali na unaweza kuelezeka. Ilikuwa hata mwanamuziki akiwa mzuri vipi akiingia kwenye bendi alilazimika kujifunza kwanza mapigo ya bendi yake mpya kabla hajaruhusiwa kutoa nyimbo mpya, hii ilikuwa ni kuratibu mtindo wa bendi.Mitindo ilikuwa tofauti hata uchezaji wake. Wakati nikiwa Vijana Jazz tuliwahi kupiga pamoja na Msondo Ngoma, wakati huo OTTU. Wapenzi wa pande zote mbili walikuwa wanasema wanashindwa kucheza staili ya bendi pinzani. Utakubaliana na mimi kuwa wakati Vijana ikipiga mtindo wa Takatuka ni muziki tofauti na Pambamoto ya Mary Maria au Bujumbura, na ni tofauti na Saga Rhumba ya enzi ya VIP, kwa hiyo majina hayo hayakuja tu , kulikuwa…

Nawaachia wananchi waseme

Image

Vijana Jazz Baada ya Maneti

Image
Ushindani uliokuwepo kati ya Maquis Original na Vijana Jazz ulikuwa mkali sana mwanzoni mwa miaka ya tisini hasa kwa ajili ya siku ya Jumapili ambapo Vijana walikuwa Vijana Kinondoni, wakati Maquis wakiwa kwenye ukumbi wao wa Lang’ata Kinondoni. Muda wa maonyesho yote mawili ulikuwa uleule hivyo kila kundi lilikuwa linatafuta kila njia ya kumpiku mwenziwe.Vijana Jazz iliamua kupata wanamuziki wengine wapya. Hapo akaingia Suleiman Mbwebwe toka Sikinde,Jerry Nashon toka BIMA, Benno Villa kutoka Sikinde lakini wakati huo akitokea Nairobi, Rahma Shally kutoka Sambulumaa, wote hao waimbaji. Shaaban Dogodogo akitokea Nairobi (solo gitaa), Mhando (keyboards), Ally Jamwaka tokaSikinde (tumba).Hapo ndipo ilipoanza Pambamoto Saga Rhumba. Ujio wa TP Ok jazz ulibadilisha sana mtizamo wa bendi kimziki. Ok Jazz , wakiwemo wakongwe wote kasoro Franco, maana hii ilikuwa baada ya kifo chake. Ingawaje walikuja na kijana mmoja ambae alikuwa anaimba kama Franco pia alikuwa anapiga gittaa kama Franco , wa…

Tancut Almasi awamu ya kwanza

Image
Mwaka 1986 wafanyakazi wa Kiwanda cha kuchonga Almasi cha Iringa chini ya Jumuiya yao ya Wafanyakazi (JUWATA), waliamua kukubaliana na mzungu mmoja tajiri wa almasi kuwa wao wamchongee almasi katika kipindi kifupi hivyo kufanya overtime na ile pesa ya overtime awaletee vyombo vya muziki. Kwa msaada wa wanamuziki waliokuweko pale Iringa, akina Mamado Kanjanika, Juma Msosi, Saidi Kananji waliweza kuchagua kupitia catalogues walizopata vyombo aina ya Yamaha. Ninauhakika bendi ingekuwa Dar es Salaam ingechagua Ranger FBT, kwani kilikuwa kipindi cha ukichaa wa Ranger hasa baada ya Mzee Makassy kupata vyombo hivyo.Vyombo vilifika na kuanza kutumiwa na wanamuziki waliokuwepo wakati ule. Uongozi wa Bendi ulimuita Ndala Kasheba kuja kuzindua vyombo hivyo na ikiwezekana kuiongoza bendi, Kasheba alifika Iringa lakini wakashindana masharti na uongozi wa kiwanda cha Tancut. Pamoja na kuwa alikuwa mwenyeji wa Iringa John Kitime alikuwa anapiga muziki Dar es Salaam ndipo alipoitwa nyumbani kujiunga …

Mlimani Park Orchestra

Image
Mlimani Park ilianzishwa mwaka 1978,ikiwa na wanamuziki kama Abel Balthazar (solo na second solo), Muhiddin Maalim Gurumo(muimbaji), Cosmas Thobias Chidumule (muimbaji), Joseph Mulenga(Bass), Abdallah Gama (rhythm), Michael Enoch (Saxophone), Hamisi Juma(mwimbaji), George Kessy(kinanda), Haruna Lwali(Tumba), ikiwa chini ya TTTS (Tanzania Transport and Taxi Services). Mwaka 1983 shirika hilo lilipopiga mueleka kifedha kama mashirika mengi wakati huo bendi ikawekwa chini ya himaya ya Dar es Salaam Development Corporation (DDC).Chini ya uangalizi wa mwanamuziki mkongwe king Michael Enoch ambaye atakumbukwa kuwa alikuwa mpiga solo hatari sana wa Dar Jazz enzi za mtindo wao Mundo (mpaka akapewa sifa ya King), bendi ilinyanyuka ikiwa na sauti ya kipekee na mpangilio wa vyombo uliofanya bendi ilitikise jiji. Michael Enoch ambaye mpaka mauti yake alijulikana pia kwa sifa ya Ticha kutokana na kufundisha wanamuziki wengi na pia kuweza kupiga vyombo vingi, alikuwa ndie kiongozi wa Bendi kwa miak…

Patrick Pama Balisidya

Image
Jina Patrick Balisdya halitakuwa geni kabisa kwa wadau wa blog hii,lazima roho zimeanza kuwadunda kama inavyokuwa kwangu kila nikimkumbuka Blai. Patrick Pama Balisidya alizaliwa Mvumi Dodoma tarehe 18 April 1946. Kabila lake alikuwa Mgogo , kabila ambalo lina wanamuziki wengi maarufu kutokana na muziki kuwa sehemu muhimu ya maisha ya kabila hilo. Mama yake alikuwa anapiga kinanda kanisani na hivyo basi kutokana na asili ya kabila lakena pia kutokana na mama yake, hakika huyu angeweza kujisifu kuwa muziki uko katika damu yake.Mdau mmoja alitutaarifu kuwa Balisidya alikuwa kiongozi wa Bendi ya shuleni kwake Dodoma secondary School. Ambapo kutoka hapo alijiunga na Chuo cha Ufundi , na baada ya kumaliza mafunzoalifanya kazi hiyo kwa muda na 1967 akawa tayari anapiga muziki Dar Es Salaam Jazz B. Kufikia mwaka 1970 Patrick alikuwa ameanzisha kikosi chake mwenyewe Afro70, kikiwa na mtindo wake Afrosa.Alikuwa mbunifu katika muziki wake, na kwa muda mrefu alikwepa sana kuingia katika wimbi la …

Jiving

Image
Katika aina ya muziki ambao ulisababisha bendi kuanza katika mashule, ilikuwa ni aina ya muziki na kucheza ulioitwa 'jiving'. Shule nyingi zilikuwa na vikundi hivi, sekondari za kike na kiume zilishindana katika jiving. Muziki huu ulikuwa umetoka haswa Afrika ya Kusini. Siasa zikaingilia kati katika miaka ya mwishoni ya sabini na kuuwa jiving katika mashule mengi. Jiving ilikuwa inaambatana mara nyingine na filimbi kama alivyokuwa anapiga Spokes Mashiyane. Mbaraka Mwinyshehe ni matokeo ya muziki huu alikuwa bingwa wa kupiga filimbi. Pichani ni kikundi cha jiving cha Mkwawa High School The Skylarks Jiving Group, akiwemo mwandishi maarufu Danford Mpumilwa (watano toka kushoto) ambaye pamoja na kuwa mwimbaji wa Bendi ya shule hiyo Mkwawa Orchestra, aliendelea mpaka kufikia kuwa na bendi yake mwenyewe pale Arusha.

Bendi za wanafunzi mashuleni

Image
Katika miaka ya sitini na sabini shule nyingi za sekondari zilikuwa na Bendi (bendi ya magitaa), hata pale Chuo Kikuu Mlimani palikuwa na Bendi nzuri tu katika kipindi hicho, Kuna Bendi za shule nyingine zilipata umaarufu wa Kitaifa kama vile Bendi ya Shule ya Sekondari Kwiro ambayo iliweza kurekodi nyimbo zake Radio Tanzania. Niongelee shule moja nadhani itatoa changamoto ya kupata habari za bendi za namna hiyo katika shule nyingine. Pale Mkwawa high School Iringa ,kulikuwa na bendi mbili. Moja ilikuwa ikipiga muziki wa kiswahili ambayo ilikuwa na wanamuziki kama Sewando kwenye solo, Masanja kwenye rythm, John Mkama Bass,Manji,Danford Mpumilwa mwimbaji, mpiga tumba kwa sasa ni Askofu moja mashuhuri, wakati huo huo bendi ya pili ilikuwa na mwimbaji machachari Deo Ishengoma akiimba nyimbo za James Brown. Bendi hii ilikweza kurekodi RTD pia vibao kama Wikiendi Iringa na Ulijifanya lulu na kadhalika. Dar Es Salaam pia palijaa bendi nyingi za shule na mitaani. Azania, Tambaza ni kati ya …

Swali la Leo

Bendi gani iliimba wimbo- Mali ya mwenzio sio mali yako? Na dongo lilikuwa likielekezwa kwa nani?

Chinyama Chiyaza

Image
Tangazo jingine la dansi la miaka hiyo ambalo nina uhakika litaleta kumbukumbu kwa wapenzi wa Maquis wa enzi hizo za Mtindo wa Telemka Chekecha Scania LBT III, wakati huo gari za Scania ndizo zilikuwa maarufu nchini na Scania LBT III ilikuwa gari yenye saiz kubwa kuliko zote, na ndio yenye kusifika zaidi, karibuni tena wapenzi wa White House mchangie, mambo yalikuwa mazito chini ya uongozi wa Chinyama Chiyaza ambae alikuwa mpiga Saxophone katika bendi. Wakati huu Maquis ilikuwa na maendeleo makubwa sana ya kuwa na mashamba, magari, matrekta na hata kuwa na Kota zake pale Sinza Palestina. Hebu angalia majina yaliyopo katika bendi.