YOUTUBE PLAYLIST

Friday, February 26, 2010

Wana Bantu Ngoma wanakula miziki

Bantu Group chini ya Komandoo Hamza Kalala imekwisha toa wakali wengi katika anga la muziki hapa Tanzania. Komandoo mwenyewe ana historia ndefu ikiwemo ya kuwa moja wa waanzilishi wa Bendi ya Vijana chini ya mkongwe John Ondolo Chacha. Amekwishapitia bendi kama Matimila na kushiriki vibao vikali kama Alimasi, amepitia UDA na ikawa katika anga za juu kimuziki Tanzania wakati wake. Komandoo hatasahauliwa na vibao alivyopiga Vijana kama Mary Maria , mpini wake wakati wa Pambamoto Awamu ya pili haujarudiwa tena. Kibao chake Nimekusamehe lakini sitakusahau cha Washirika Stars ni picha tosha ya kazi za Hamza. Pichani ni Juni 1, mwaka 1996. Kwenye onyesho kubwa la Siku ya Mazingira ambalo ndilo lilikuwa onyesho la kwanza la muziki 'live' kuonyeshwa na ITV. Na lilirushwa kwa muda wa masaa kama 6 wananchi wakipiga simu lilendelee hewani!!!!. Wasanii kama MR2 walipata umaarufu mkubwa baada ya tamasha hili pale Mnazi Mmoja. Tamasha liliendeshwa na CHAMUDATA chini ya Mwenyekiti John Kitime.
Picha ya chini tunamwona watatu toka kushoto Eddy Sheggy, na mwishoni ni Rogart Hegga ambaye kwa sasa yuko Twanga Pepeta.

7 comments:

  1. Anonymous23:27

    Bwana Kitime umesikia kama Mzee mwenzio Hamisi Kitambi amefariki?
    mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete
  2. Hiyo habari ndiyo unanitaarifu. Kama ni kweli ni masikitiko makubwa kwangu naomba MUNGU amlaze pema peponi

    ReplyDelete
  3. Anonymous18:00

    Mkuu,

    Umesikia kwamba mdau mkubwa wa Blog hii Mheshimiwa Patrick Tsere ameteuliwa kuwa Balozi wetu nchini Malawi?

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli nichukue nafasi hii kumpa hongera Mheshimiwa kwa hilo. Wanamuziki wa Tanzania wanapendwa sana Malawi, miaka michache iliyopita nilihudhuria Miss Malawi na wimbo wa Mr Nice wa Kuku kapanda baiskeli ndio ulikuwa ukipigwa wakati mabinti wakipita mbele yetu ilikuwa eh eh duuu. Haya, tutamwomba Balozi wetu atutangaze vizuri isiwe kama ubalozi wetu Marikani ambapo kwenye website ya serikali wameandika kuwa Zouk na Ndombolo ni muziki wa kiasili wa Tanzania.

    ReplyDelete
  5. Anonymous18:29

    Mkuu,

    Wakati mwingine kunakuwa na mambo ya ajabu sana. Mchana wa leo nilikuwa namsikiliza mwanamuziki wa Malawi Mzee Wydham Chechamba katika album yake ya Chechamba's Piano & Guitar Sounds. Halafu jioni nikapata habari za uteuzi wa Muheshimiwa Patrick Tsere kuwa Balozi wetu nchini Malawi. Nami hali kadhalika naomba kupitia bloguni kwako nimpe Muheshimiwa pongezi za dhati kwa uteuzi huu.

    Nilipata kusoma presentation ya wakili mmoja wa Tanzania aliyekuja ughaibuni kuzungumzia mambo ya hati miliki. Nilitamani kulia. Ninayo kopi ya hiyo presentation lakini sijui iko wapi! Sasa siyo ajabu hata kidogo tovuti ya ubalozi wetu kuandika Zouk ni muziki wa Kitanzania.

    ReplyDelete
  6. ukitaka ujue kama ndombolo ni muziki wa asili wa Kitanzania na spargheti ni chakula cha asili cha Watanzania nenda tovuti ya Ubalozi wetu USA http://www.tanzaniaembassy-us.org/tzepeo.html..nimewaandikia wakajibu watanijibu mpaka leo jiii

    ReplyDelete
  7. Anonymous12:45

    Tunasikitika kifo cha mzee wetu Hamis Kitambi. Hii habari ya website ya ubalozi wetu Marekani inanitia kichefuchefu hata kabla sijaiona... naishia hapo.
    Rich Mloka

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...