Vijana Jazz Band wakisubiri kupiga muziki katika siku ya kumpokea Mzee Nelson Mandela mara baada ya kuachiwa kifungoni, hapa wakiwa stadium Morogoro. Toka kushoto waliosimama John Kitime kwa sasa yupo Kilimanjaro Band, Marehemu Agrey Ndumbalo, Mhasibu wa Bendi, Abou Semhando yupo African Stars (Twanga Pepeta),Marehemu Fred Benjamin, Said Mnyupe yuko Msondo,Said Mohamed Ndula, Rashid Pembe anendelea na muziki Mak Band, Hassan Show yupo Malasyia na Kinguti System wakipiga muziki huko. Waliokaa mpenzi wa bendi, marehemu Bakari Semhando, Juma Choka yupo sikinde.

Picha ya chini, Mohammed Gotagota, Freddy Benjamin,Mhando,Said Mohamed 'Ndula',Rashid Pembe,Aggrey Ndumbalo, hiyo ndo Vijana Jazz Saga Rhumba

Comments

Anonymous said…
Kitimeeeee! nakumbuka enzi hizo miwani yako ilikuwa inanyufa kibaoooo
John Mwaipopo said…
nakumbuka siku hii kama jana vile. nilikuwepo hapo uwanjani jukwaa la nyuma ya picha. nakumbuka vilivyo kida waziri alipochengua jukwaa kabla ya mzee nelson kuingia kiwanjani akiwa nyuma ya defender pamoja na rais mwinyi na mama winnie madikizela mandela.mwe!

Popular posts from this blog

Marijani Rajabu

SITI BINTI SAAD

Western Jazz Band

Sikujua kama utabadilika - Simba wa Nyika

Mlimani Park Orchestra

Super Kamanyola ya Mwanza