Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Wednesday, February 3, 2010

Taarab
Muziki wa Taarab unautata wa vyanzo viwili. Kuna wanaosema taarab iliingia nchini mwetu kupitia ikitokea Mombasa. Kuna tafiti nyingine ambazo zinaonyesha Sultan Barghash wa Zanzibar aliwapeleka wanamuzikiwawili Misri kujifunza upigaji wa Taarab,na hao waliporudi ndo walipanda mbegu ya Taarab nchini mwetu. Taarab imekuwa nahistoria ambayo ya kuwa na aina nyingi za taarab, na mpaka leo mabadiliko ya taarab yanaendelea. Imefikia sasa kuna hata vikundi vya taarab vina wacheza show. Taarab imekuwa pia ni ya kucheza na si kusikiliza ujumbe tu kama ilivyokuwa zamani

3 comments:

Anonymous said...

Mkuu,

Tunaweza kukubaliana mabadiliko katika kila kitu kwamba hata binadamu ana mabadiliko ya marika yaani utoto, ujana, umakamo, uzee hatimaye ukongwe. Mabadiliko haya ya kimaumbile hayamfanyi mtu/binadam abadilike kuwa ngedere. Lakini si vyema kumfananisha au kughafilisha wasifu wa mtu/mwanadamu na ngedere. Kwa sababu mtu/mwanadamu asilani atabaki kuwa mtu/mwanadamu hali kadhalika ngedere asilani atabaki kuwa ngedere.

Taarab ni taarab na huu muziki mpya ambao bado haujapata jina kamili iwe ni mipasho au rusha roho utabakia kuwa rusha roho au mipasho na asilani huwezi kuwa taarab.

Kuhusu maswali uliyouliza yanaweza kujibiwa na tafiti nyingi kuhusu muziki wa Taarab zilizoandikwa na kurekodiwa na taasisi na watafiti mahiri wa muziki(Outstanding Musicologists)kama vile kina Said A.M. Khamis, Werner Graebner, Mohamed El-Mohammady Rizk, K.M. Askew, Global Music Centre na vyuo vikuu mbali mbali hususani vya Ulaya na Marekani.

ZAIDI: Said A.M. Khamis anapagawishwa na mabadiliko katika nidhamu ya muziki wa Taarab - Wondering About Change: The Taarab Lyric and Global Openness.Nordic journal of African Studies 11(2): 198-205 (2002). Said A.M. Khamis* University of Bayreuth, Germany.
(http://www.njas.helsinki.fi/pdf-files/vol11num2/khamis2.pdf).
Nadhani Bwana Said A.M. Khamis tupo kwenye upande mmoja wa mtazamo kwamba hii iliyokuja sasa ni mipasho au rusha roho ni aina nyingine ya muziki na siyo taarab.

John F Kitime said...

Ni kweli Mkuu wengi wanapagawishwa na mabadiliko yanayoendelea ambayo yanatokana na sababu nyingi, lakini pia ni vizuri kujiuliza kama taarab "halisi" ni ipi ambayo ndicho kipimo cha taarabu

Anonymous said...

Mkuu,

Kipimo changu cha taarab halisi kinaanzia kwenye tungo (Ushairi wenye vina na maudhui au hata kama ni bashrafu ni bashrafu iliyopigika katika mtindo na ala za okestra ya taarab). Tofauti nyingine imelalia kwenye muziki wa Taarabu: kimuziki (ala zitumikazo, mtindo wa muziki unaopigwa kimapigo (Rhythm), ghani (melody), na mwafaka (harmony).

Halafu linakuja suala la nidhamu ya muziki wa taarab: Mtindo wa utumbuizaji wa muziki wa taarab (presentation style) kuanzia wajihi wa wanamuziki (performers personalities), muundo ukaaji jukwaani (stage arrangement), mtindo wa jukwaani na majukwaa (stage setting and arrangement), mazingira ya utumbuizaji (performance aura), wahudhuriaji na aina wahudhuriaji onyesho (audience and audience target/ audience demography). vigezo hivyo nilivyovitaja na vinginevyo ndivyo vinavyoitofautisha taara na chakacha au na mipasho au rusha roho. Kabla ya mipasho na rusha roho palikuwepo chakacha lakini haikuwahi kutokea kuchanganya taarab na chakacha. Au siyo?

Haya mambo ndiyo ya kutaka serikali ya sultani iteue Sultani mwanamke. Ikishateuliwa Sultani mwanamke huo si usultani tena. Au Vatikani wamchagua Papa mwanamke, ikitokea kuchaguliwa papa mwanamke huo si Ukatoliki tena. Vivyo hivyo ikiwa kama taarabu itapigwa kwa ala za muziki wa dansi, na wacheza shoo tena shoo hizi za kiwana mipasho, na tungo zisizo za kishairi na maneno yasiyo na staha, na kupigwa kwenye kumbi za vilevi basi hiyo si taarab ni mipasho au rushaa roho na si taarab.

Hebu niambie leo ukute watu wanapiga muziki wao kwa kutumia accordian, gitaa baridi na manyanga halafu wakuambie hii ni heavy metal, utaafikiana nao au utafikiri wamepatwa na ugonjwa wazimu?

Adbox