YOUTUBE PLAYLIST

Thursday, February 18, 2010

Orchestra Makassy katika moja ya awamu zake nyingi, baadhi ya wanamuziki hapa wapo jijini Dar es Salaam wakishughulika na mambo mbali mbali. Wakati huu Mzee Makassy alikuwa na vyombo vipya aina ya Ranger ambavyo vilipata umaarufu sana baada ya Franco na TP OK jazz kuja navyo katika ziara yao moja hapa Tanzania. Pichani ni Mzee Makassy anashughulika na kueneza injili na muziki wa injili. Mbombo wa Mbo mboka pia amefuata nyayo za Mzee Makassy na ni fundi maarufu wa vyombo vya muziki,Vivi, Malik,Kiniki Kieto,Seye Star,Ilunga,Shinga wa shinga,Tchimanga Assossa Kiongozi wa Bana Maquis, Okema, Marehemu Mzee Simaro (Aimala Mbutu) Baba mkwe wa Luiza Mbutu, Halfan Uvuruge, King Ray, Micky Jagger Jagger, Yusuph, Magoma Sony. Hapa ni enzi ya Jamani msinicheke kufilisika,

11 comments:

  1. Anonymous20:08

    Mkuu,

    Nyimbo ya Namolema au Mosese ya Mzee Makassy ilipata kuchukua tuzo VOA. Naomba utupe habari zaidi za album ya AGWAYA. Naomba tuchekie data na Emmanuel Muganda wa VOA utupe habari kamili na sahihi.

    AGWAYA nadhani ndiyo album pekee kuipuliwa jikoni na kuingia sokoni kwa wakati ule. Mwaka 2005 imetolewa tena kwenye CD katika series ya Legends of East Africa Orchestra Makkasy The Original Recordings chini ya lebo ya ARC. Ile timu iliyotengeza album ya Agwaya ilikuwa kama timu ya Basketball ya Marekani iliyoenda Olimpiki Barcelona, Spain mwaka '92. Nilihudhuria onyesho lao Mkirikiti Bar, Msasani walipotoka Mwanza lilikuwa linasisimua kuanzia shoo ya Hanifa na Angelika wa Kupenda kwenda kwa waimbaji Mzee Makassy, Franscois Makassy Jr, Tshimanga Assossa, Athumani Kindiya, Nduka Masingu nadhani na wale mapacha halafu magitaa ya kina Uvuruge, Aimala Mbutu hadi kwenye wapiga tumba na drums na brass section ilikuwa moto wa kuotea mbali.

    Mbali na albam ya Agwaya aliwahi pia kutoa 45" ya Mke wangu ambayo baadaye Remmy Ongala alikuja kuirekodi na Orchestra Super Matimila. Mkuu, tafadhali ukiweza tuletee historia ya Super matimila kuanzia enzi za Mosesengo Fanfan hadi Remmy Ongala na Cosmas Chidumule.

    Orchestra Makassy Niliwaona mara ya kwanza Airwing Ukonga wakiwa na kina Marehemu Isiaka Molai Gobii na Remmy Ongala akiwa mpiga tumba. Baaday wakawa wanapiga kila Jumapili mchana Bwalo la Polisi Oyster Bay ( Kwa historia ya Bwalo la Polisi Oyster Bay ukimpata Afande Chico nadhani ni RPC Kilimanjaro kwa sasa).

    Keep it Bro kazi nzuri saanaaaa, hongera mnoooo!

    ReplyDelete
  2. Anonymous23:15

    John! kwakweli unataka kututoa roho wazee wa enzi hizo kwa maelezo haya fasaha na historia ya ukweli ya muziki wa dansi tanzania. sidhani kama kuna kati ya vijana wa kizazi hiki atakae weza kuja kueleza yanayojiri katika enzi hizi wakati huo ujao maana hakuna ama hawana.
    Hapo juu nimefurahi sana kujikumbusha tangazo la enzi hizo enzi tuliowasha moto kwa kugonganisha mawe lakini uliwaka kweli kweli.
    najaribu kumkumbuka marehemu Aimalambutu simaroo baba wa Farijala mbutu "bezist" wa kilo hasa baada ya kutoka kwa makassy na kujiunga na Bicco stars bendi ambayo ninaamini ndipo lipomalizia uhai wake. Sijui kama King Ray uliyemtaja ni yule Ray thomas mpuliza trumpet wa zenji?
    Any way nakutakia kheri katika kila unalolifanya katika blog hii

    ReplyDelete
  3. Anonymous03:33

    Mzee Kitime,

    Kwa kwa kwenda na mada naomba kuuliza, je, ni kweli Dr. Remmy Mtoro Ongara ni mpwa wa Mzee Makassy? Na ni kweli kwamba Remmy aliletwa Tanzania na Mzee Makassy?

    Nimeuliza hayo ili kupata connection ya Dr Remmy kuanza kupigia muziki wa dansi bendi ya Makassy mara alipoingia Tanzania kwa mara ya kwanza mwishoni mwa miaka ya 70, kama sikosei alikuja 1977 or 1978.

    Mimi nilikuwa mshabiki sana wa bendi yako ya zamani ya TANCUT Almasi iliyokuwa na makazi yake pale Iringa mjini. Nyimbo zenu nyingi za wakati huo mpaka sasa huwa ninapenda sana kuzisikiliza.

    Je, ukiwa kama mmoja wa wana bendi ya TANCUT zama hizo, unaweza kuomba kibari cha ku-reproduce nyimbo hizo kwenye CD na kuziingiza tena sokoni?

    Kwa kuwa wewe umekuwa mdau mkuu wa hakimiliki na haki shirikishi, je, kwa bendi ambazo zilirekodi nyimbo zao kwenye studio za RTD miaka hiyo, ni nani mwenye haki nazo, ama ambaye ana final decision? Kwa kuwa hapo ninaona kuna watunzi, wamiliki wa bendi, waimbaji na pia studio iliyorekodi. Nina amini kwamba kama kungekuwa na uwezekano wa kutoa matoleo mapya ya nyimbo za zamani zingepata sana soko ili mradi kuwe na udhibiti wa mauzo ya hizo kazi ili kuzuiwa makanjanja wanaozalisha CD majumbani na kuziingiza mitaani.

    Mwisho kabisa, nakumbuka umeimbia pia bendi ya Vijana na Ruaha International. Je, hukuwa hukuimba na wale vijana wa kule Mafinga Jones Corner (Wana Kimulimuli) au maarufu kama Mafinga JKT.

    ReplyDelete
  4. Uncle Kitime. Mimi naweka ombi jingine. Nalo ni kuhusu hawa kina UVURUGE. Wako ama walikuwa wangapi na kwa wale wanaofahamu mlipo, mtujuvye hawa watu wako wapi?
    Kina Maneno, Halfan na wengine.
    Tafadhali

    ReplyDelete
  5. King Ray ni marehemu alikuwa mpulizaji saxaphone,na alikuwa ni kiongozi wa bendi ya Makassy

    ReplyDelete
  6. Anonymous15:39

    John
    napata wakati mgumu sana kuamua nianze na kipi katika mengi niliyonayo kichwani hasa kuhusiana na muziki wa hapa kwetu.

    Kwa kuwa wewe uu mwanamuziki wa kiwango cha kutukuka katika kizazi hiki, kwa namna ya kipekee ningeomba utupatie historia fupi ya jamuhuri jazz.

    kila mara ninapo hudhuria onesho lenu la bendi ya the kilimanjaro (wanan njenje) ninasikiliza vitu vingi wakaki mkiwa jukwaani.
    Sasa ninalotaka toka kwako ni ufafanuzi kuhusu ubora wa sauti hasa ukizingatia kwamba nyakati zile kulikuwa hakuna sound effects na jamaa wale wa jamuhuri waliweza kujipanga na kusukuma sauti ambazo mpaka wa leo sidhani kama kunawakushindanishwa nao.

    Pia nyakati zile studio zilikuwa za kiwango cha nyakayi zile . Sipati picha wangekuwa wana nasa sauti kwa vyombo hivi vya kileo kama pangetosha. Hizi kelele zinazoitwa "miziki" za vijana wa leo zisinge sikika kabisaa.

    Pia hebu nijuze? TANCUT almasi ni nini siri ya wao kuwa na vyombo vya YAMAHA ambavyo mpaka sasa sijaviona sokoni. Je lilikuwa ni chaguo la nani? na nikweli Marehemu kasheba ndiye aliyevichagua? pia nitafutie mzee hugo kisima ninataka nijue kama ile mixer yake yenye chnl nyiiingi aliiiza wapi ?? ni kumbukumbu tosha FBT

    ReplyDelete
  7. Patrick Tsere16:03

    Ndugu yangu Michuzi asante sana. Unajua baadhi yetu kama mzee Kitine, huenda tulizaliwa mapema kabla ya muda wetu ambao ni sasa. Ndiyo maana hatuwaogopi vijana wala hatuwapigi vita. Hata mindset zetu ni za kileo. Kwa hio kila teknology inapobadilika hatutishiki wala hatuikimbii. Nakumbuka miaka ya nyuma wakati ndiyo masuala ya internet ndiyo yanaanza kuwa commercialised nilikuwa na bosi wetu mmoja ambaye mimi na Balozi Peter Kalaghe tulikuwa tumemshawishi ofisi yetu nayo iwe na facility ya internet. Siku moja yule bosi wakati wa mkutano akatulaumu sana tunapoteza muda wa ofisi kwa sababu siku nzima tunautumia kucheza computer games. Uelewa wake wa teknolojia ulikuwa ni kwenye computer games kama vile Nintendo na kadhalika. Tukamwambia yule bosi "wewe badala ya kutusifu kuwa siku nzima tunatafuta information kwenye internet wewe unafikiri sisi tunacheza Nintendo". Hayo ndiyo mambo ya generation gap.

    I am happy siku hizi hatunao mabosi wa aina hiyo japo hawana raha wala amani na teknolojia. Hebu niambie mabosi wangapi wanazo blackberry au simu zinafanana na hiyo ambao wanazitumia hizo simu kikamilifu and optimally. Wengi hata kutuma sms mgogoro. Watoto wao wakichezea na kubadilisha configuration wamekwama. Hahaha.

    ReplyDelete
  8. Anonymous18:53

    Kakaaa

    Nje ya mada kidogo - Hivi yule mwanamuziki SLIM ALLY nadhani alikuwa mkenya aliimba wimbo wa 'You can do it' ambao marehemu kaka yangu alikuwa anaupenda sana na akiupiga kwenye 'CHENJA' yake unaweza kufahamu habari zake? Tafadhali tujuze.

    Mdau

    Muddy

    ReplyDelete
  9. Kuhusu Jamuhuri Jazz wana Dondola, vijana wa barabara ya 17 Tanga, maelezo yaja yatambatana na ya watoto wa barabara ya 4 Atomic Jazz wana wa Kiweke , usihofu. Ukweli ni kuwa sound effects zilikuweko na zilitumika sana kwenye uimbaji na magitaa hasa gitaa la solo. Na kila bendi ilijitahidi kuseti na aina yake ili kitakachotoka kiwe tofauti na bendi nyingine, ndo maana hata ukisikia sauti ya gitaa la Atomic ni tofauti na Jamuhuri. Effect ambazo zilikuwa maarufu wakati huo zilikuwa repeater(hasa aina ya Dynachord),Michael Vicent wa Urafiki na hata Michael Enoch(King Michael) enzi za Dar Jazz alitumia sana effect hii. Echo chamber na reverb pia zilikuwa maarufu kwa ajili ya waimbaji,Cry baby(au Wah wah pedal) kama aliyotumia Balisidya katika solo la nyimbo ya harusi ilitumika sana na hasa na bendi za vijana.
    Tancut orchestra ilianza na vijana wa pale pale Iringa, akina Mamado Kanjanika, Juma Msosi, Amani Ngenzi na wao ndo walitumia catalogue walizozipata mahala kuchagua vyombo hivyo.Kasheba aliitwa kuzindua bendi na alikaribishwa kujiunga wakashindana masharti alipoomba kupewa nyumba kama ya meneja mkuu wa Tancut na gari kama lake.
    Mafundi katika studio za zamani walikuwa na training ya kweli ndio maana kazi zao ni bora kuliko kwenye studio za kisasa, pili mpaka leo imekubalika kuwa recording ya analogue inautamu ambao digital haiufikii, kiasi cha kwamba wanamuziki wakubwa maarufu hufanya recording kwenye digital na kuingia gharama ya kufanya mastering kwenye teknolojia ya zamani ya analogue.

    ReplyDelete
  10. Du raha ya blog hii ni kuwa unakumbushwa mengi sana naikumbuka hiyo santuri ya You can do it ambayo Slim Ally aliimba akiwa na Hodi Boys, ilikuja kipindi cha style ya bumping na tuliicheza sana, sishangai kaka yako kuirudia tena na tena tulikuwa wengi. Niliyonayo kuhusu Slim ni yafuatayo; Slim Alli alizaliwa Mombasa December 1947 akaanza kupiga muziki akiwa High school iliyoitwa Hamisi Secondary School. Alianza na Kitale Hotel Band badae Tusker Band kabla ya kujiuynga na Hodi Boys bendi ambayo ilianza 1966 ikiwa na wanamuziki kama Geoffrey Ngao, Nick Kim na Henry Nbagho walikuwa hasa wanapiga nyimbo za Otis Redding na Percy Sledge. Slim aliacha bendi na kuzunguka nchi nyingi hadi aliporudi Kenya mwaka 1976,akawakusanya tena Hodi Boys na kurekodi album“You can do it”.

    ReplyDelete
  11. Anonymous08:46

    Kakaaa

    Shukran sana na tuko pamoja

    Mdau

    Muddy

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...