Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Friday, February 5, 2010

Mzee Humplick aliwahi kupigwa marufuku

Je unajua kuwa Mzee Frank Humplick ambaye ndiye mtunzi wa nyimbo kama Chaupele Mpenzi, Embe dodo imelala mchangani, aliwahi kutunga nyimbo iliyopigwa marufuku na kusakwa nyumba hadi nyumba ili kusibakie hata nakala ya wimbo huo? Maneno ya wimbo huo yalisema hivi:
Uganda
nayo iende

Tanganyika ikichangaruka, Kenya na Nyasa zitaumana

Nasikia fununu wanavyoichanachana China, Kitisho!

I am a democrat, I don't want communism, English, Yes, No I don't know, Kizungu sikijui

Wanyika msishindane na Watanganyika

Wimbo huo ukaanza kutumika kabla ya mikutano ya Mwalimu Nyerere na kuanza kuwa maarufu kama wimbo wa kudai uhuru, wakoloni haraka sana wakaona wimbo huu utaweza kusababisha vurugu kama ambazo zilikuwa zinaendelea Kenya chini ya Maumau. Serikali ikaupiga marufuku na kuanza kuusaka nyumba hadi nyumba

2 comments:

Anonymous said...

hizo ndio historia tunazo taka kaka thanks alot for bringing this
Kasesela

TANCOMPUTER said...

Hawa kina mzee Humplick ndio walikuwa watunzi hasa wa nyimbo za muziki, sijui sasa kama tunaweza kupata watunzi kama hawa, ok labda kwa kuwa muziki nao unategemea na kizazi. Bado sijaona wanamuziki wanaoweza kupambana na kina Mbaraka Mwinshehe, Salum Abdalla, Marijani Rajab nk.
Hongera Kitine kwa kuanzisha blog inayotukumbusha wanamuziki wa zamani.

Adbox