YOUTUBE PLAYLIST

Monday, February 1, 2010


Matangazo ya Bendi zamani yalikuwa yakipambwa na vituko mbalimbali. Wakati huo matangazo yalikuwa yakitoka katika magazeti tu. Na magazeti yalikuwa hayana teknolojia ya kutoa picha za rangi. Hili ni tangazo la bendi ya Maquis ambayo kwa wakati huo ilikuwa na wanamuziki karibu hamsini

3 comments:

  1. Nakumbuka wakati nimeanza kufuatilia matangazo yao, nilikuwa nashangazwa saana na utayarishaji wao. Yaani suala la Graphic Design halikuwa akilini. Nakumbuka picha za kila msanii na zana yake. Wa Tarumbeta anayo, wa Sax anayo, wa Gitaa vivyo hivyo, waimbaji na mic zao.
    Dah!! Sijui tumepoteza nini katika HISIA NA TOUCH YA MUZIKI NA WANAMUZIKI WETU????
    Umenikumbusha mbaali sana Uncle
    Asante

    ReplyDelete
  2. Mjomba hapa umenikumbusha mbali sana. Rafiki yako kipenzi alikuwa mpenzi sana wa haya mambo na mpaka leo kuna santuri zake nyingi na vipande vya matangazo alivyokuwa anatunza.

    Please fanya mpango wa kunitafutia mashine ya kuchezea hizo santuri maana ni nyingi na nina hamu ya kusikia tena muziki wa miaka ile ilikuwa na ladha gani nikiwa na umri huu.

    ReplyDelete
  3. Nikifika tu ntakwambia tuonane, nimenunua na software ya kuhamishia hizo santuri kwenye computer ili uzihamishie kwenye CD. Halafu lile feni nimepandisha juu, haliwezi kukukata tena shingo we njoo nyumbani

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...