YOUTUBE PLAYLIST

Thursday, February 4, 2010

Mara nyingine mtu unaweza kuanza kupata picha kama vile wanamuziki wako Dar es Salaam tu, jambo ambalo si kweli. Japo ukweli ni kuwa zamani kulikuweko na Bendi karibu kila wilaya nchini. Hapa ni bendi 2 kutoka Dodoma. Super Melody na Saki Stars.
Mwenye gitaa na jaketi la rangi mbili ni Mzee Ikunji, huyu pamoja na kupigia bendi kama Tabora Jazz pia alikuweko Tancut Almasi Orchestra na ndie aliyepiga second solo kwenye nyimbo kama Masafa Marefu, Nimemkaribisha nyoka, na Kashasha

2 comments:

  1. mkubwa John Kitime kwanza nakupongeza kwa kazi hii yako ya kujitolea kuufafananua na kuleta kumbukumbu ya muziki wa tanzania.

    swali langu ni hili. mie napenda sana muziki lakinni muziki sio fani yangu. nadonoa moja hapa na lingine pale. Hivi mnaposema second solo mnakuwa na maana gani. ninapohudhuria live bands huwa naona magitaa matatu. yaani bass, rhytm na solo (sijui hili ndio first solo?). naomba kujua kwa lugha nyepesi tu hili second solo ni nini.

    ReplyDelete
  2. Mtindo wa kuwa na kitu kinaitwa second solo ulianzishwa na DR Nico na mdogo wake Dechaud. Katika mfumo huo kunakuwa na magitaa yafuatayo , Bass, Rythm, second solo au wenyewe waliliita mi solo na solo. Hili lilikuwa na sauti kati ya solo na rythm, na kazi yake ni kuhama kumuunga mkono solo na mara nyingine kumunga mkono rythm. Kwa kweli baada ya hapo wanamuziki waliaanza kufanya ubunifu mbalimbali na upangaji wa muziki kwa kutumia mfumo huu, na wengine kama Kilaza waliboresha na kuongeza gitaa la 5 wakaliita Chord Guitar. TP Ok Jazz waliboresha tena na kufanya Mi solo kuwa solo kamili hivyo kukawa na wapiga solo wawili katika nyimbo moja. Vijana Jazz katika album yao ya VIP walifuata mfumo huu katika Nyimbo kama VIP, Thereza, Bahari Imechafuka na hata album iliyofuata wimbo kama Shoga umepangwa katika mtindo huo. Hivyo Shaban Wanted na Shaaban Dogodogo walikuwa wote wanapiga solo kwa wakati mmoja kwa wimbo uleule. Katika mfumo huu mazoezi makali ni lazima ili isiwe fujo bali mpangilio.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...