Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Wednesday, February 3, 2010


Kati ya mwanamuziki Mtanzania ambae historia hajamtendewa haki kutokana na kutothaminiwa kwa kazi zake ni marehemu Mzee Frank Humprik. Mzee Humprik anaeonekana hapa katika picha ya rangi ameishi kwa miaka mingi ya mwisho wa maisha yake Lushoto. Mzee huyu akiwa na dada zake wawili walitikisa anga za muziki wa Afrika ya Mashariki, na bado wanaendelea kufanya hivyo japo hawatambuliwi kabisa. Kundi lao lililoitwa Frank na dada zake waliuletea ulimwengu nyimbo kama Embe dodo imelala mchangani, Kolokolola, Chaupele Mpenzi na nyingine nyingi ambazo bendi bado zinapiga nyimbo hizo mpaka leo na baadhi ya wanamuziki wamekuwa wanazirekodi bila hata kutaja mtunzi wa nyimbo hizo. Mbaya zaidi mara nyingi nyimbo hizo zimekuwa zikitambulishwa kama nyimbo za mwanamuziki mwingine kutoka Kenya marehemu Fundi Konde.
Mzee Fundi Konde ambae hapa chini yuko na mwanamuziki mwingine maarufu wa Kenya Fadhili William aliyeimba Malaika, ndiye aliyetuachia nyimbo kama Ajali haikingi, Mama Leli, Wekundu si hoja, Mombasa siendi tena na kadhalika

1 comment:

Anonymous said...

Mwezi November 2009 (mwaka jana) alifariki Mzee Joseph Ojiki. Kama kawaida ni kwamba hakuna hata bendi moja, wala TFF, au magazeti yoyote yaliyoandika makala za kumuenzi zaidi ya kwenye mablog ya Father kidevu na Michuzi.

Nini ambacho kinafanyika kuwaenzi kina Mzee Ally Sykse, David Mussa, Bi Shakila na wengineo? Zama zile za Kilimanjaro Hotel ya yule Meneja Muhindi Kadu waliibuliwa kina Fadhili William na Fundi Konde. Leo ni zama ya TBL, ZAIN, VODACOM, TIGO, TCC nk nini kinafanyika zaidi ya kuwaleta Mahiphop na mafiesta ya bongoflava ambapo ingewezekana pia kupata ufadhili wao kuwaenzi wanamuziki wa zamani na kuudumisha rhumba la Kitanzania ambalo lingeweza kuwa na soko kubwa zaidi duniani kuliko huu muziki wa kisasa ambao umepungukiwa vigezo kadhaa vya kuweza kuuweka kwenye ushindani wa soko la kimataifa.

Adbox