Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Tuesday, February 16, 2010


Kati ya Bendi ambazo Mzee J Mwendapole aliziendesha kwa muda mrefu ni Afriso ngoma. Hiyo ilikuwa bendi yake, ikawa na wanamuziki kama Maida na Belly Kankonde, iliweza kurekodi nyimbo kadhaa, lakini bendi hii iliongezeka umaarufu alipoingia marehemu Lovy Longomba, wakati huo akiwa na akina Kinguti system, Anania Ngoliga, Toffy Mvambe, Salim Shaaban Malik Nduka Masengo(Maliky Star) hao wakiwa waimbaji, Solo Gitaa- John Maida, Peter Kazadi, Robert Tumaini Mabrish, Rythm- Mjusi Shemboza, Bass-George na Kasongo, Drum -Ayub Karume, Abdul, Tumba- Magoma Sony, Trumpet-Juma Urungu, Ramadhani, Mbaraka Othman. wengi kati niliowataja wametangulia mbele ya haki. Baada ya hapo aliwahi pia kuwa na bendi ambayo ilikuwa na wanamuziki kadhaa kutoka sikinde ikawa inaitwa Sikinde Academia, ambayo haikudumu sana. Baada ya hapo amekuwa msaada mkubwa wa kuwasaidia wanamuziki wengi vyombo wakati wananzisha bendi zao.
Pichani ni Marehemu Lovy Longomba

4 comments:

Born 2 Suffer said...

Asante kwa blog yako unatuletea habari nzuri za wanamuziki wa zamani,Na karibu sana.

Anonymous said...

Lovy Longomba na Awilo Longomba ni ndugu? Mzee Vicky Longomba walikuwa na mahusiano naye?

John F Kitime said...

thanx

Anonymous said...

Hongera, nina mengi ya kuyajua toka kwako, hongerea sana nimevutiwa

Adbox