YOUTUBE PLAYLIST

Tuesday, February 2, 2010


Jerry Nashon aka Dudumizi, moja ya waimbaji na watunzi mahiri waliowahi kupita katika anga la muziki Tanzania, nyimbo zake nyingi kama Imakulata (Bima Lee), Thereza, VIP (Vijana Jazz) zilimuweka katika matawi ya juu katika enzi zake

5 comments:

  1. Anonymous19:00

    R I P Jerry,kazi yako nilikua ninaikubali sanaa,bingwa alikua juu sana,lakini ndio hivyo,wanasema kizuri sikuzote hua hakidumu,sasa haupo tena duniani,pumzika kwa amani Nashon.Mdau London.

    ReplyDelete
  2. Hapa umetukumbusha mbali sana, mshkaji alikuwa na sauti ile mbaya..oh dudumizi kifo hakina huruma, nasikia historia alikufa kwa ajali ya pikipiki

    ReplyDelete
  3. Moses Gasana17:17

    Jerry Nashon alikuwa mahiri.Sauti yake nzito sana ilikuwa(Crooner).Wimbo Imakulata ni mtamu sana kaka Kitime laiti kama ungeuweka hapa kidogo watu wausikie na kufahamu umahiri wa marehemu Nashon ingekuwa poa sana.
    Je aliacha familia?

    ReplyDelete
  4. Jerry aliwahi kupata ajali mbaya ya pikipiki katika maisha yake yaliyosababisha aondolewe bandama, lakini alifariki baadae kwa ugonjwa tuu.Sijawahi kusikia kama aliiacha familia

    ReplyDelete
  5. Ndugu Moses Gasana, wimbo huu waweza kuusikia hapa (http://www.eastafricantube.com/media/9547/Jerry_Nashon_and_Bima_Lee_Orchestra_-_Makulata/) japo ubra wake si wa juu sana.
    Kaka kitime afanyacho ni zaidi ya zawadi kwetu wapenda muziki huu.
    Asante kwa mara ya tena na tena.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...