Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Wednesday, February 10, 2010

Hemed Maneti


Hemed Maneti mwanamuziki muimbaji aliyetokea Cuban Marimba na kutua Vijana Jazz mpaka kifo chake. Wimbo wa mwisho aliyorekodi uliitwa Nelson Mandela uliyotungwa na John Kitime. Wimbo huo ulitungwa ili kupigwa radioni wakati Mzee Mandela alipokuwa anatembelea Tanzania mara baada ya kuachiwa toka gerezani. Hakupanda tena jukwaani baada ya kurekodi wimbo huo.

20 comments:

Baraka Mfunguo said...

Binafsi nimekuwa nikivutiwa sana na nyimbo za zamani. Ingawa wakati huo nakiri nilikuwa bado mdogo. Nakumbuka ushindani baina ya Hemedi Maneti na Marijani Rajab.
Binafsi wimbo wa CHIKU aliouimba Maneti ninaupenda sana. Enzi ya CHAKACHUA.

TEKNOHABARI WEBMASTER K.A.P said...

Sasa kitine ilitakiwa huo wimbo wa Nelson Mandela ulitakiwa uwepo hapo chini ili tunapata story na kuusikiliza. Ungeweka kwenye youtube halafu ukachukua embeded code ukaweka hapa ili mambo yaende vizuri.

John F Kitime said...

Baraka umenichanganya kidogo, sikumbuki ushindani kati ya Maneti na Marijani kwa kweli, maana walikuwa ligi tofauti kila moja kivyake, na kuhusu wimbo Chiku, zilikuweko nyimbo mbili za Chiku ambae ndie alikuwa mke wa Maneti na wakazaa mabinti wawili mapacha, aliziimba wakati yuko Vijana Jazz na si Chakachua amabo ulikuwa mtindo wa Bendi ya Urafiki, iliyokuwa mali ya kiwanda cha nguo cha Urafiki.

Anonymous said...

John mwakitime aka mzee nyongise!
Nimefurahi sana kupata nafasi ya kusoma mamboz kwenye blog yako. najua uko nje ya nchi kwa wakati huu lakini pokea zangu pongezi.
Natamani sana siku moja ukiwa na bendi yako ya wana Njenje unikumbushie kibao chako cha "nyongise" hata kikiwa katika kahadhi ya mduara itapendeza.
Vile vile ninakuomba kama kuna uwezekano mujiunge tena pamoja kwa maana ya akili zenu wana njenje. najua wakati huo ulikuwa hujajoin group, mutukumbushie zile za zamani kama "karibu kwenye jiji dar" najua itakuwa kazi but tuzisikie kiduuuchu.
Mwezi march ni wakati wenu wakuwa mahali fulani mkifanya "uzalishaji" This time msifanye makosa. Tunataka mafanikio zaidi ya kinyaunyau. nawatakia kheri wooote.

Baraka Mfunguo said...

Nakumbuka Marijani alipewa jina Sauti ya Chiriku lakini alipokuja Maneti ikasemekana yeye ndiye anayestahili jina hilo na Marijani kuitwa jabali la Muziki. Kama nitakuwa nimekosea mkuu unisahihishe.

Patrick Tsere said...

John ninakumbuka mwaka 1988 marehemu Maneti akiongozana na vijana jazz walikuja Lusaka baada ya kukaribishwa na chama cha UNIP enzi hizo Mzee Kaunda akiwa bado Rais wa Zambia. Wakati huo mimi nilikuwa Afisa wa Ubalozi ambaye unaweza ukasema ndiyo nilikuwa mwenyeji wao. Kiongozi wao wa msafara alikuwa Mheshimiwa said Thabit Mwambungu ambaye sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Morogoro.

Pamoja na kuwa ziara hiyo ilifana lakini Maneti alikuwa ameishaanza kudhoofu na alitokea jukwaani mara moja tu. Pamoja na kuwa kabla ya hapo alikuwa hanifahamu ilibidi nimchukue nyumbani kwangu ili kumpatia matibabu na matunzo ya ziada. Wakati tukiongea alinieleza hofu na mashaka juu ya maradhi yake. Nilichofanya ilikuwa ni kumfariji na kumtia moyo.

Wakati huo walipokuja walirekodi nyimbo zao kwenye studio lakini wakati wanaondoka waliniomba niwachukulie master copy ya nyimbo zao. Kwa kweli kwa moyo wa uaminifu baada ya kukabidhiwa hiyo copy niliwapelekea. Sipendi kujisifu lakini ingekuwa siku hizi sina uhakika kama mtu mwingine angeonyesha uaminifu niliouonyesha mimi. Maana mwingine angetumia ile copy kutengenea kanda au cd na kuuuza. Sisi wa kizazi cha Azimio la Arusha bado maadili tunazingatia.

Mwaka 1989 November nilkuwa Dar nikaenda pale Mango kule kwenye ukumbi wa nyuma nikawakuta Vijana Jazz wanapiga muziki. Maneti naye nilimkuta. Tukaongelea juu ya kifo cha Franco ambacho kilikuwa kimetokea October. He was not comfortable with Franco's death. I knew he was psychologically affected.

All in all iko siku sisi sote tutakuja kufa na hatuna sababu ya kuhofia kufa. Kifo siyo laana wala balaa.Kwa uhai na uzima tulionao sasa ni kila mmoja wetu kwa nafasi yake atimize wajibu na tuishi na binadamu wenzetu vizuri.

John F Kitime said...

Bwana Baraka ndo nasikia toka kwako,najua kuwa Marijani alikuwa anaitwa Chiriku na maneti akaja kuitwa hivyo lakini sikusikia kulikuwa na ugomvi wa kugombea jina. Najua wote walijipa majina ya kifaransa kwenye mwaka 1983 na majina hayo pamoja na wimbo Bomoa tutajenga kesho wa orchestra Mambo Bado, na jina Power Savimbi ambalo alikuwa anatumia mwanamichezo mmoja na pia stageshow, vilipigwa marufuku na Umoja wa Vijana mkoa wa Dar es Salaam, kwa wakati huo Umoja huo ulikuwa na uwezo wa kufanya hayo.

Moses Gasana said...

Patrick Sere umetoa kumbukumbu nzuri ila pia ya kutia simanzi kwa kuwa inaongelea kipindi cha kuumwa kwa Maneti.
Mie nilikuwa mdogo sana wakati huo na hata sasa nikitaja umri wangu huenda mkanicheka lakini naomba niseme kuwa muziki wa bendi na wanamuziki kama Maneti na Marijani nawakubali sana hadi leo.Ninapomsikiliza Maneti akiimba katika nyimbo kama Maria,Aza, na nyinginezo, loh natamani kulia.Natamani kama angekuwa hai.
Maneti alikuwa gwiji kweli kweli wa uimbaji.Na pia kikoso chake na vijana kama Wanted,Adam Bakari, Eddy Sheggy walikuwa mahiri kweli.
Mungu azirehemu roho zao jamani
Moses Gasana
City University London

Moses Gasana said...

Kaka Kitime naomba kuuliza.Hao watoto wa marehemu Maneti wapo wapi? na wanafanya nini sasa?hawajambo na ni wenye furaha?

John F Kitime said...

Maneti alikuwa na wtoto kadhaa mmoja wapo anejulikana kama Maneti ni mcheza mpira mahiri Dar Es Salaam, ana binti ambae alizaa na Kida Waziri yuko katika afya nzuri pale Arusha, kuna utata kuhusu hali za wale mabinti mapacha aliozaa na mkewew Chiku, mara ya mwisho ilisemekana wako Sumbawanga sina taarifa juu yao kwa miaka mingi, japo ni changa moto nitafuatilia.

Anonymous said...

Mzee Tsere umetupa hint nzuri sana. Mimi pia nilikuwa mdogo sana lakini nilikuwa nafuatlia sana hasa albamu ile ya NA NAI yenye nyimbo MASAKI,NA NANI,STELLA nk.

Kaka Kitime tuwekee nyimbo hizo japo kwa mistari.

Mzee wa Changamoto said...

Woooow!!!!
Uncle Kitime nimekuwa nakuheshimu kwa kazi zako jukwaani na hata nje ya jukwaa. Na hapa (ambapo kwa bahati mbaya nimepagundua leo) pameongeza HESHIMA kwako. Lakini pia pameniongezae ujuzi.
Nakiri utoto / udogo enzi ambazo Tanzania tulikuwa na MUZIKI WETU WA KUJIVUNIA. Lakini nilikuwa naufuatilia saana na hata sasa nina baadhi ya rekodi zao.
Hemedi Maneti alikuwa mmoja kati ya watu waliofanya niipende Vijana Jazz. N kwa kuwa hapa ni kumhusu yeye, basi wacha nijikite kwake. Bahati mbaya hakuishi muda mrefu tangu niwe na mamlaka ya kumsikilza. Kazi zenu zilikuwa na bado zaheshimika maishani mwangu. Bado nasikiliza bila kuchoka kazi kama Aza Umeniumbua, Mama wa Kambo, Ngapulila, Ogopa Tapeli, Penzi Haligawanyiki I & II na hata Mwisho wa Mwezi.
Alipotutoka Maneti nikahisi Eddy Sheggy angekamata mikoba. Naye aliondoka kabla "sijaifaidi" kazi yake. Lakini kaze Zake alizofanya Washirika Tanzania Stars na hata Bima Lee huendelea kunifariji. Lakini baada ya "kuukimbia Muziki halisi uliowapa heshima" na kuingia kwenye "dansi ya kisasa" na Uncle Hamza Kalala, hapo nili-lose touch nao na bado nauliza tulipojipoteza (http://changamotoyetu.blogspot.com/2008/09/ni-kipi-tulichopoteza-kwenye-muziki.html)
Hata leo bado nasikiliza muziki ule kuliko wa sasa. Bado nafurahia kusikiliza nyimbo zenu kama Samahani ya Uongo, Helena Mtoto wa Arusha, Ngoma za Afrika, Butinini, Lutandila, Masafa Marefu, Imma, Fundisho, Shibe Kijijini nk kuliko nyimbo zilizotoka miaka 2 iliyopita hapo nyumbani. Nyimbo zetu za sasa ni "disposable".
Kinachoniuma ni kuwa HAKUNA ANAYEWAENZI WATU WALIOTUMIA NA WANAOTUMIA MUDA NA AKILI ZAO KUENDELEZA KILICHO CHEMA KWETU. Na sikitiko hili niliwahi kuliandika hapa (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/08/ni-lini-tutawaenzi-watu-hawa.html)
Binafsi nilijitahidi kuuenzi muziki wa Dansi na nilianzisha kipengele maalum kuenzi muziki huu kwenye blog yangu, lakini host wa muziki wangu (imeem.com) walipotea miezi kadhaa iliyopita, hivyo sina namna ya ku-stream nyimbo hizo.
Lakini sasa naamini nimepata PAMOJA PA KUSHIRIKI HISIA ZA MUZIKI HUU NA WANAMUZIKI WETU.

Patrick Tsere said...

John sijui suala hili unaliangalia vipi. Kuna watu wengine mpaka leo hii hawafurahii technology ya keyboard na computers bado wanaona typewriter ndiyo ilikuwa kifaa hasa. Mimi jamani huu mtindo wa siku hizi wa kwenda kwenye matamasha kuwasikiliza performers ambao wanatembea na CD zao siyo siri I hate it and I feel cheated. Muziki niaoupenda ni ule unakutana na live performance kama wanavyofanya Njenje, African Stars. Hata nikiwa kanisani, haki ya Mungu, kikianza kipindi cha sifa ambapo sisi waumini hatuimbi bali tunawasikiliza hao wasanii wa gospel music. Kila wanapoanza mimi huchukuwa biblia yangu na kujisomea. Unamkuta msanii kapanda juu ya stage anayo microphone halafu anaiambia studio "track number moja tafadhali". Hivi pale anaimba nini kwa kweli si kudanganyana tu? Anyway sijui walitazamaje hilo. Vipaji vya uhakika ni vile ambavyo live band inakuwepo. Au uzee unaniponza na ninaonekana out of date? Hiyo ni teknolojia ya shortcut na ujanja na ubabaishaji. Tell me nini maoni yako?

John F Kitime said...

Sijui nilie au nicheka? Nalia kwa kuwa watu wengi ambao si wanamuziki wazuri wanajipatia umaarufu kwa kutumia playback. Nalia kwa kuwa wasanii wazuri hawakubali playback na promoters wanawaona ni gharama hivyo wanatupwa pembeni. Kikubwa ni kukumbuka kuwa wasanii wakweli ndo watakaoibuka tena. Kwenye mwanzo wa miaka ya tisini nakumbuka ilikuwa hata inaandikwa kwenye magazeti kuwa bendi zitakufa kwa ajili ya umaarufu wa disco.

Mzee wa Changamoto said...

Talking about PLAYBACK.
Sijui kwanini wanaitwa wanamuziki? Nadhani tungewaita Vocalist. Na tatizo kubwa ni kuwa hawana wanalojua zaidi ya kuweka sauti kwenye nyimbo. Na kama ulivyosema Uncle Kitime, gharama zinawakimbiza na kuwatenga wajuao muziki.
Na sasa unaona waimbaji wenyewe wanakimbia gharama za kurekodi. Hakuna msanii wa "bongo flava" anayetaka kumfuata Uncle Kitime, Uncle "Pangamawe" ama Mzee Mabera amsaidie kumuwekea kionjo cha gitaa. Hakuna anayeweza kumfuata Uncle Kepi kumuomba Bassline. Hakuna hata anayeweza kumfuata Uncle Kanku Kelly kuomba percussions ama Uncle Mafumu kupata Sax ama kumfuata Uncle Mng'ande kumuomba mdomo wa bata. Na hawa ni wachache kati ya wengi wenye uwezo wa KUKUZA MUZIKI WETU. Vyote wanataka wavipate kwenye "keyboard". Matokeo yake ni kuwa "muziki" hauwezi kuchezeka popote (zaidi ya redio zao wanazohonga). Nilisikia instrument ya Sisi Tambala ambayo ilinunuliwa (kama sio kuombwa) na wasanii wa nje ya nchi na wakaweka vocal. Sounds REAL. REAL TANZANIAN MUSIC ikiwa na marimba, ngoma na vitu vingine vingi.
Kibaya zaidi ni kuwa hata wasanii wanakimbia studio zenye kuwapa ubora, wanaenda kuleee ambako studio ni kinanda na kuta imezungushwa magodoro asubuhi hiyohiyo.
TUNAJIPOTEZA KATIKA HARAKATI ZA KUJITAFUTA.
Labda TUTAFIKA SIKU MOJA

Patrick Tsere said...

John umenisaidia kuelezea hisia zangu haswa kuwa "sijui nilie au nicheke". Ukweli dawa iko kwa wasikilizaji na audience wanaokubali kwenda kwenye so called matamasha hayo. Nilipokuwa Mkuu wa Wilaya Ilala nikiwa bado mgeni kwenye kazi hiyo nilihudhuria one of the tamashas kama mgeni rasmi. Ilibidi nifanye jitihada za ziada za kidiplomasia kuonyesha kupendezewa kwangu na show ile. Baada ya kuhudhuria nyingine moja I made a quiet decision never to attend any. Nikisikia msondo wako nilikuwa naenda kwa hiari yangu kabisa. Unajua ikabidi mimi na Mheshimiwa Kandoro ili tusionekane kama vile tunapenda matanuzi, tulijiwekea utaratibu wa kuhudhuria kila function yenye muziki wa msondo. Kwa sababu pale unaona wazi vipaji na jitihada za musician wetu. Kwenye play back nikiitwa nilikuwa natafuta "official reasons" za mimi kushindwa kuhudhuria.

Mimi naamini live performance bado inayo future nchi hii. Ila naomba unieleweshe how easy is it to obtain loan financing kwa ajili ya kukuza muziki. Kwa vile wanamuziki nao siyo wajasiriamali? Kama ndivyo how easy is it for them kupata fedha za mkopo?

Michuzi said...

JFK sijaona khabari ya 'Dudumizi' mkuu. Tunaomba upekue makabrasha yako tumuenzi...Gerry Nashon.

Mh. Patrick Tsere ahasante kwa kumbukumbu na hongera kwa uaminifu wako, japo siku hizi ungeonekana 'fala' kwa kurejesha pochi ulilookota. Wewe ni mfano wa kuigwa. Nafurahi kuwa nilibahatika kufanya kazi nawe ulipokuwa Idara ya wakimbizi na baadaye Mkuu wa Wilaya ya Ilala. Pia nakusifu kuwa miongoni mwa wazee wachache wanaokwenda na wakati. Mambo ya teknohama unayajua nje ndani. hongera...

Patrick Tsere said...

Ndugu yangu Michuzi asante sana. Unajua baadhi yetu kama mzee Kitine, huenda tulizaliwa mapema kabla ya muda wetu ambao ni sasa. Ndiyo maana hatuwaogopi vijana wala hatuwapigi vita. Hata mindset zetu ni za kileo. Kwa hio kila teknology inapobadilika hatutishiki wala hatuikimbii. Nakumbuka miaka ya nyuma wakati ndiyo masuala ya internet ndiyo yanaanza kuwa commercialised nilikuwa na bosi wetu mmoja ambaye mimi na Balozi Peter Kalaghe tulikuwa tumemshawishi ofisi yetu nayo iwe na facility ya internet. Siku moja yule bosi wakati wa mkutano akatulaumu sana tunapoteza muda wa ofisi kwa sababu siku nzima tunautumia kucheza computer games. Uelewa wake wa teknolojia ulikuwa ni kwenye computer games kama vile Nintendo na kadhalika. Tukamwambia yule bosi "wewe badala ya kutusifu kuwa siku nzima tunatafuta information kwenye internet wewe unafikiri sisi tunacheza Nintendo". Hayo ndiyo mambo ya generation gap.

I am happy siku hizi hatunao mabosi wa aina hiyo japo hawana raha wala amani na teknolojia. Hebu niambie mabosi wangapi wanazo blackberry au simu zinafanana na hiyo ambao wanazitumia hizo simu kikamilifu and optimally. Wengi hata kutuma sms mgogoro. Watoto wao wakichezea na kubadilisha configuration wamekwama. Hahaha.

MUDY 4RM DSM said...

KAKA KITIME NIME SIKILIZA MZIKI KTK ILE PLAYER YAKO, OFCOARSE NIME VUTIWA JE NAWEZA KUJA NA FLASH YANGU UKA NITILIA ILI NIWE NASIKILIZA, AU NAWEZA KU DOWNLOAD?

Anonymous said...

Naomba kuuliza, hivi Hemedi Maneti hakuacha mtoto?

Adbox