Jukwaa la wapenzi wa mambo ya muziki wa Tanzania-

Breaking

Saturday, February 6, 2010

Enzi za Buggy

Katika miaka ya 60 hadi katikati ya 70 kulikuwa na bendi nyingi za vijana ambazo unaweza kulinganisha na wanamuziki wa sasa wanaojulikana kama kizazi kipya. Katika jiji la Dar es Salaam, kulikuweko na bendi nyingi kama vile The Sparks, The Comets, The Flames, The Jets, Crimson Rage, The Lovebugs, Trippers Imagination, Safari Trippers, Afro 70. je unakumbuka nyingine ?

17 comments:

Patrick Tsere said...

Yeah kulikuwa na Flaming Stars wengi wao wakiwa wanafunzi wa Minaki miongoni mwao akiwemo Michael Mhuto, Cuthbert Sabuni na mdogo wake John Sabuni, Peter Kondowe (Peko). Hao waliwaka sana mwaka 1966 to 1968. Wimbo wao mmoja ninaokumbuka ni "Mpenzi Maria sisahau x2 Hata nyota nazo, pia mbalamwezi haziwezi kusahau Maria. Usikuu huwa nalia usiku huu huwa naota Maaamaria". Baadaye wakaenda Mombasa and then they split.

Walikuwepo Hot Five ambayo ilikuwa kali sana miaka hiyo ya 1966 hadi 1969 ilipovunjika ikazaliwa Sparks na Tonics. Ilipokuwa the Hot 5 kiongozi wao alikuwa Michael Jackson na akina Jerry Mwakipesile na Lameck Ubwe. Kwenye drums alikuwa Adam Salumu aka Addy Sally. Ubwe alibakia na Sparks na akina Jackson na Sweet Francis na mdogo wake Green Jackson wakaanzisha Tonics ambayo ilifanya makao yake Arusha wakipiga muziki CAMEO Bar karibu na Msikiti mkuu wa arusha.

When I was in Zambia from 1984 to 1996 nilikutana na Michael Jackson akiwa kwao alikuwa ameugua kichaa wa kuzurura jijini Lusaka amebeba makopo na usingeweza kuamini kwamba ndiye yule aliekuwa star. It was a sad scene I must say.

Kipindi hicho wengine walikuwa the Rifters chini ya Adam Kinguyi, Kijana wa Ilala.

Na hao uliowataja. Of course walikuwepo wakongo kama akina Pascal Onema wakipiga New Palace Hotel ambayo sasa ni Mbowe. Akina Papa Micky na Nova Success. Freddy Supreme (Ndala Kasheba) na Fauvete

John F Kitime said...

Umetaja akina Sabuni ni muhimu usimsahau Raphael Sabuni ambae mara ya mwisho nilimuona live akiwa na STC jazz, wakiwa na Marijani Rajab, na nyimbo zao kama , Ulikuwa usiku wa manane, Rafiki si mtu mwema.
Top Life Bar Kinondoni bado ni bar, ukiangalia unashangaa kuwa palikuwa pakubwa kiasi cha bendi kupafanya ndo mahala pake, nadhani utakumbuka wimbo wa Papa Micky akisifu Top Life Bar Kinondoni

Patrick Tsere said...

Yes Yes. Kuna wimbo wa Papa Micky mpaka leo nikiusikia bado unanipa hisia kali. Nao ni Sizeline. Unajua Papa Micky ile beat aliyokuwa anaitumia kupiga solo was quite unique na katika nyimbo zake zote ilikuwa haikosekani. Hata Franco solo lake ukisikia wimbo hata kama huujui mara moja jinsi solo inavyopigwa unajua huyo ndiye Franco. The same was with Papa Micky.

Ndiyo ile niliyokuwa naisema Branding. Hivi kwa kiswahili tutaita nini.Alama ya bidhaa yako ambayo inakutambulisha kwa jamii na soko? Uzuri wa brand kwenye soko unakuwa unawalenga watu maalum. Na kwa njia hiyo unaweza kuboresha brand yako. Wale wanaopenda brand yako hawatahama na unakuta mpaka na watoto wao wanakuwa fans wako. Leo hii nikisikia Radio One kile kipindi cha sunday special yule binti mtangazaji anasema yeye alizijua zile nyimbo kwa sababu mama yake alikuwa akizicheza nyumbani kwao. Hio ndio uzuri wa brand. Nina hakika wale fans wa Njenje baada ya miaka kumi hata kama nyinyi mtakuwa bado alive nyimbo zenu hazitakosa mashabiki.

John F Kitime said...

Kama uliipenda Sizeline pia lazima unaikumbuka Maeliza. Papa Micky alikuwa anatumia effect inaitwa repeater kwenye gitaa lake la solo,kama una kumbuka hata African Quilado walikuwa wanatumia effect ya aina hiyo. Katika kipindi kile kila bendi ilijitahidi kuwa tofauti na hivyo kuwa na identity yake, hicho unachoita branding,japo branding kwenye sanaa inaweza kukupeleka kwenye monotony,lakini ni jambo muhimu ambalo bendi nyingi siku hizi hazilitilii maaanani na hivyo kuishia kugawana wapenzi na mwisho kuanza kushutumiana au maarufu kwa lugha ya vijana kuwa na bif. Wasanii wenye brand tofauti hawawezi kuwa na bif, ila sasa unaweza kutembelea bendi 3 ukaona kama uko bendi ileile.

Anonymous said...

Katika jiji la Dar es salaam miaka ya 1968 hadi 1971 kulikuwa na kundi la "Groove Makers", hawa walikuwa machchari sana katika Soul Music hasa kupiga nyimbo za James Brown na Otis Redding, je mnawakumbuka hawa ambao wengi wao walikuwa shule ya na Sekondari ya Azania na Saint Josephs?

John F Kitime said...

Kuna mheshmiwa sana mmoja ndo alikuwa mwimbaji wa Groove Makers, hakuna nyimbo ya James Brown ilikuwa inamshinda, japo kwa sasa sijui hahahaha , kwa ruksa yake nitamwomba ajitokeze au nimtaje siku moja au nitamwomba Mheshmiwa Tsere awasilane nae atatuambia mengi kuhusu wakati huo.

Anonymous said...

Kuna bendi ya BAR KEYS ya upanga (kama sijakosea ni 4 flats upanga)sikumbuki wapigaji nilikuwa mdogo sana mpaka leo kuna instumental lao naweza kulipiga kwenye kinanda

Anonymous said...

Kakaaa

Tafadhali nijuze kuhusu ile bendi ya BANANGENGE kama sijakosea walikuwa wanavaa sana enzi zao je ilikuwa inamilikiwa na nani?

Mdau

Muddy

John F Kitime said...

Hahaha kulikuweko na bendi mbili moja Barkeys na nyingine Barlocks...Funguo na kufuli. Barkeys ndo hawa Tanzanites hivyo ukiwafwata wakumbushe hiyo instrumental yao ninauhakika watafurahi ni wanamuziki wazamani sana, Barlocks ilipiga sana mwishoni Kilimanjaro Hotel na hasa bada ya Kilimanjaro Band enzi hizo wakiitwa The Revolutions kuhama pale Kilimanjaro Hotel Simba Grill. Barlocks ilikuwa na waimbaji kama Neddy Nombo ambaye ntamwomba atueleze mengine kuhusu Barlocks. Namkumbuka Martin na mdogo wake Derick wote watoto wa Upanga hao. East Coast mupoooooo?

Anonymous said...

Kulikuwa na Barkeys Seaview, Barlocks Kisutu Patel Stores opposite Daily News, na Les Strokers Upanga Mindu Street kwa kina Galinoma. Mtaa wa Jamhuri alikuwapo mzee mmoja wa Kigoa na wanawe pia alikuwa na bendi sikumbuki jina lake.

Barkeys walikuwa kina George, Abraham na Amato Kapinga, John na William Chiduo, John Mhina Vaga, Yona Mgassa, Aidan Chanai Pepe na Toroa Mohamed Toroa.

Barlock walikuwa kina Robin, Ivan, na kaka yao, Abraham vingoko, Chirwa wengine sikumbuki baadaye kina Neddy.

Les Stroker walikuwa Kipingo, Benny na Inno Galinoma, Chopeta brothers, Mambazo wengine sikumbuki.

John F Kitime said...

Aksante saaana kwa majina na information ya ziada nimejaribu kuwasiliana na wengine kama wanaweza kutupa maelezo zaidi ya wakati huo, pia picha zao thanks again

Anonymous said...

Brian Shaka and the Oshekas walikuwa Mtaa wa Undali, Upanga.

John F Kitime said...

Loh umenikumbusha Bendi yangu, The Oshekas, nilipitia pale kabla ya kujaribu kujiunga na Biashara Jazz Band chini ya Juma Ubao (King Makusa)

Anonymous said...

Mkuu,

Kumbe ulipita The Oshekas na ulijaribu kujiunga na Biashara Jazz! Samahani hivi Dunda Dunda walikuwa wakipiga Blues, Soul na Funky "kwa Kiswahili" au yalikuwa masikio yangu? Kwa sababu wakati mwingine nilikuwa nikimsikiliza King Makusa nilikuwa nasikia bridges na twanging za Blues, Soul na Funk kuliko ile mionjo ya kikwetu.

John F Kitime said...

Mpaka leo bado sijaona mwanamuziki aliyekuwa anaspidi kwenye vidole kama King Makusa. Na nimeshaongea na wanamuziki wengi waliowahi kupiga nae wamesema hivyo pia. Kuna wakati alikuwa anavaa gitaa na saxaphone na mbele yake kuna kinanda anachopiga waulize Makonde Bar Msasani watakwambia, huku pembeni akiwaa na mpiga bezi Brittish na drummer Chamchu

Anonymous said...

Mkuu,

Asante sana kumbe siyo mimi pekee yangu niliyekuwa nasikia vile. Halafu kulikuwa kuna ile nyimbo moja siikumbuki vizuri aliyokuwa anasema maneno haya "..Mshenga alisemaa ..karibu tena bwana weee.." Duuh, ile nyimbo ndiyo uthibitisho wa speed ya vidole vya King Makusa na rollings za Drummer Chamchu.

Asante sana tena sana kwa kumbukumbu hii.
Nalikumbuka lile chama la King Makusa na mtindo wake wa kupiga vyombo vingi kwa wakati mmoja na huku anaimba.

Anonymous said...

Napenda kuwakumbusha groupe moja ya vijana wa Kigoa iliyokuwa ikiburudisha Kilimanjaro Hotel,George De Souza pia kundi lingine ambalo lilitamba sana na nikiwa mpenzi wao,The Sunburst.Mengine mengi tutakumbushana siku za mbele.

Adbox