YOUTUBE PLAYLIST

Sunday, February 7, 2010

Bendi Zetu

Tanzania tuna bahati mbaya ya kutokuweka kumbukumbu nyingi sana. Kati ya hizo ni kumbukumbu za bendi gani au vikundi gani vya muziki viliwahi kuweko. Labda tusaidiane kila mmoja wetu ajaribu kukumbuka ni kikundi gani kilikuweko wilayani kwake nianzae na mifano michache
******
Iringa-
Highland Stars
Tancut Almasi Orchestra
Chikwala chikwala
Ruaha International
Vico Stars
Mkwawa Orchestra
******

Morogoro
La Paloma Jazz
Cuban Marimba
Morogoro Jazz
Les Cubano
Vina vina Orchestra
******

Ifakara
Sukari Jazz
Kilombelo Jazz
Malinyi Jazz
Kwiro Jazz
Mahenge Jazz
******

Tanga
New Star Jazz
Jamuhuri Jazz
Atomic Jazz
Tanga International
Amboni Jazz
******

Tabora
Tabora Jazz
Nyanyembe Jazz
Kiko Kids haya tuendelee
******

Mwanza
Orchestra Super Veya
******

Moshi
Orchestra Zaire Success
Bana Africa Kituli
********

Mpwapwa
Mpwapwa Jazz
******

Dodoma Jazz
Dodoma International
Materu Stars
Saki Band
Super Melody
*****

Songea
Tembo Jazz
Orchestra Sere sere
******

Lindi
Mitonga Jazz
******

Masasi
Kochoko Jazz

9 comments:

  1. Moses Gasana16:25

    Kaka Kitime, hatuwezi weka Matimila mkoa wa Ruvuma/Songea? maana nakumbuka kusikia RTD kipindi fulani kuwa bendi hiyo ilianzia huko kabla ya kuhamia Dar.
    Moses Gasana

    ReplyDelete
  2. Ni kweli bendi ilianza Songea iliitwa kwanza Orchestra Selesele, we mngoni?

    ReplyDelete
  3. Anonymous17:41

    TX Seleleka, Iringa.

    D.O. Misiani and Shhirati Jazz, Musoma baadaye Kenya.

    ReplyDelete
  4. Anonymous16:27

    Mwishoni mwa miaka ya '70 nilinunua Biography ya Salum Abdallah Yazide pale Dar es Salaam Bookshop. Nadhani ndiye mwanamuziki pekee wa Tanzania ambaye historia ya maisha yake imeandikwa na kuchapishwa. Sijui kama kitabu kile kinapatikana hadi sasa?

    ReplyDelete
  5. Nakikumbuka kitabu hicho kilikuwa na cover ya light blue na picha ya Salum Abdallah ambayo ndi iko kwenye hiyo video. Nilikosea na kumwazima mtu kopi yangu sijaipata tena,nimekuwa nakitafuta kila mahala sijakipata. Kama ntapata taarifa kilipo ntaitundika hapa

    ReplyDelete
  6. Anonymous20:35

    Haswaaa, ndiyo hicho hicho. Cha kwangu kipo sehemu fulani nyumbani lakini sijui wapi?

    Mkuu,

    Ngoma Iko Huku ina video yake? Zilipotoka Ngoma Iko Huku na Masimango nilizitia mkononi siku chache baada ya kuwa released. Nilipofika nyumbani nilikuwa nazisikiliza kwa kurudia rudia kwa masikuu kadhaa.

    PS/
    Unaweza kufahamu kwa nini Best hits za Marijani hazijatengezewa CD? David Mussa na Mzee Ndabagoye wakiombwa watakataa?

    ReplyDelete
  7. Ntaongea na huyu mjerumani aliyetoa masimango na salum abdallah, lakini najua kuna complication, si hits zote alizoimba Marijani ni zake, kwa mfano Georgina ulikuwa na wa Uvuruge pengine hilo ni tatizo

    ReplyDelete
  8. Anonymous21:11

    Tofauti na Mbaraka na Salum Abdallah ambao walimiliki bendi zao, Marijani alikuwa mwajiriwa katika bendi zote alizopigia. Trippers ilikuwa ya David Mussa kama sikosei na Dar International ya Mzee Ndabagoye. Sasa hapo sijui makubaliano yao kuhusu hati miliki ya miziki alikuwa anabakia nayo nani mwenye bendi au mtunzi?

    Michuzi aliwahi kutoa tangazo kwamba Mzee Ndabagoye karidhia kurekodi miziki ya Dar International kama kuna mdau mwenye nia. Check out na Michuzi atakupa contact za Mzee Ndabagoye. Ismaili Kaka yake Michuzi alikuwa insider wa Dar International huyu naye anaweza kuwa link nzuri.

    PS/
    Mkuu,

    Unaonaje kama utatoa shindano la kuchagua Top Ten Tanzanian Hits of All Time?

    ReplyDelete
  9. Ntamtafuta Michuzi na bahati nzuri huyo kakake ni mtu tunafahamiana. Unajua hata Mbaraka haikuwa rahisi hivyo maana katika nyimbo za Morogoro Jazz kulikuweko nanyimbo za watunzi wengine kama Marehemu Mzee Abdul Mketema, Kulwa Salum na wengineo kwa hiyo nakumbuka wakati niko Chamudata tuliwapelekea wanamuziki wengine na warithi wao pesa za masimango hadi Morogoro vijini, ila ilikuwa rahisi kwa zile za Super Volcano maana ile ilikuwa bendi yake na maamuzi yako mikononi mwa familia yake.

    ReplyDelete

SAFARI ZANGU NA BENDI sehemu ya kwanza.

  TANCUT ALMASI ORCHESTRA  wakiwa Jamhuri Stadium Dodoma   Sikumbuki ni safari ngapi za kimuziki nilizowahi kuzifanya hapa nchini katika m...