Posts

Showing posts from February, 2010

Swali la Leo

Swali la leo......... Bendi gani ilipiga wimbo wa Banchikicha? Kwa msaada tu bendi hiyo ilishinda mashindano ya Bendi Bora Tanzania 1973

Kina nani hawa?

Image
Leo natoa picha 3 za wanamuziki maarufu wakati wakiwa bado makinda, swali ni akina nani hawa?

Mzee Hamisi Kitambi Hatunae Tena

Image
Mzee Hamisi Kitambi hatunae tena. Amefariki tarehe 26 Feruary 2010, na kuzikwa tarehe 27 February 2010. Mzee Hamisi Kitambi kwa mara ya mwisho alikuwa bendi ya Msondo Group. Mungu Amlaze pema peponi.(Picha kwa hisani ya ya www.issamichuzi.blogspot.com)

Wana Bantu Ngoma wanakula miziki

Image
Bantu Group chini ya Komandoo Hamza Kalala imekwisha toa wakali wengi katika anga la muziki hapa Tanzania. Komandoo mwenyewe ana historia ndefu ikiwemo ya kuwa moja wa waanzilishi wa Bendi ya Vijana chini ya mkongwe John Ondolo Chacha. Amekwishapitia bendi kama Matimila na kushiriki vibao vikali kama Alimasi, amepitia UDA na ikawa katika anga za juu kimuziki Tanzania wakati wake. Komandoo hatasahauliwa na vibao alivyopiga Vijana kama Mary Maria , mpini wake wakati wa Pambamoto Awamu ya pili haujarudiwa tena. Kibao chake Nimekusamehe lakini sitakusahau cha Washirika Stars ni picha tosha ya kazi za Hamza. Pichani ni Juni 1, mwaka 1996. Kwenye onyesho kubwa la Siku ya Mazingira ambalo ndilo lilikuwa onyesho la kwanza la muziki 'live' kuonyeshwa na ITV. Na lilirushwa kwa muda wa masaa kama 6 wananchi wakipiga simu lilendelee hewani!!!!. Wasanii kama MR2 walipata umaarufu mkubwa baada ya tamasha hili pale Mnazi Mmoja. Tamasha liliendeshwa na CHAMUDATA chini ya Mwenyekiti John Ki…

Vumbi

Image
Kwa wapenzi wa Maquis Original jina la "Vumbi" ni la kutia kumbukumbu nyingi sana, na kwa wale ambao wamekuwa wakiusikia ule wimbo wa Chatanda Ngalula walisikia tena na tena Tchimanga Assossa akilitaja jina hilo wakati Vumbi anacharaza gitaa tamu la solo kwenye wimbo huo. Vumbi kwa sasa anaendelea na muziki huko Sweden na maelezo ya maisha yake kimuziki ni haya. Jina lakekamili ni Alain Kahanga Dekula , alizaliwa katika jimbo la Kivu katika Jamhuri ya Kongo. Baada ya kumaliza High School alianza kupiga gitaa katika bendi ya Bavy National iliyokuweko Uvira Kusini mwa Kivu. Baadae akiwa na kaka yake Rachid King wakajiunga katika bendi ya Grand's Mike Jazz Band wakati huo ikiwa na wanamuziki kama Remmy Ongala,Kasaloo Kyanga,na Kawele Mutimanwa. Akaja Tanzania na kujiunga na Orch.Maquis Original na kati ya nyimbo ambazo anajulikana nazo sana ni Ngalula and Makumbele.Wakiwa na mtindo wa Zembwela-Sendema,alikuwa jukwaa moja na miamba wa magitaa wakati huo akina Nguza Viking &q…

Tumkumbuke Chakubanga

Image

Historia fupi ya muziki wa dansi

Ukitaka kuongea muziki wa dansi uliingiaje nchini ni muhimu kujua historia ya mji wa Tanga. Tanga ndipo muziki wa dansi ulipoingilia nchini. Wajerumani waliusambaratisha mji wa Tanga kwa mizinga kati mwaka 1888 na 89. Na baada ya hapo kuujenga upya kwa kufuata mpangilio uliosababisha Tanga kuwa na mitaa maarufu kama barabara ya kwanza ya pili na kuendelea. Wajerumani walianzisha shule ya kwanza ya serikali Tanga 1892 na hapohapo wakanzisha bendi ya shule ya kwanza, pamoja na kuwa Wajerumani hawakutawala muda mrefu baada ya hapo lakini Waingereza waliiendeleza sana bendi hiyo iliyokuwa ikipiga aina mbalimbali za muziki wa kigeni. Dansi ilianza kwanza kama klabu ambapo watu walialikana kuja kucheza aina mbalimbali za muziki wa kizungu mtindo maarufu unaojulikana kama ballroom dancing. Aina hizi za klabu zilianzia Mombasa na kuingia nchini kupitia Tanga na kisha kuletwa Dar Es Salaam na klabiliyokuwa maarufu Tanga iliyoitwa Tanga Young Comrades Club, klabu nyingine ilianzishwa ikaitwa Ne…

Jerry Nashon aka Dudumizi

Image
Nimeweza kumpata mtu ambae ndiye aliyemlea Jerry Nashon kimuziki na haya ndo aliyoniambia kuhusu Jerry. Nae si mwingine bali ni Bwana Ruyembe ambae kwa sasa ni kiongozi pale Baraza la Sanaa la Taifa
Jerry alikulia Musoma Mjini kijiji kiitwacho Kigera kilichopo Halmashauri ya Manispaa ya Musoma jirani na shule ya Sekondari Mara. Nilikutana naye mara ya kwanza akiwa Musoma Catholic Mission club ambayo leo ni Mwembeni secondary School akiwa anajifunza kupiga gitaa. Alikuwa ana mazoea ya kwenda kwenye hiyo social club ya kanisa iliyowaunganisha vijana wanamichezo mbalimbali. Nilimchukua katika Bendi yangu niliyokuwa nimeiunda muda huo 1980s ikiitwa Special Baruti Band. Nilimuunganisha na Mpiga rhythm wangu akiitwa Charles Koya ambaye hivi sasa anapiga na Bendi ya Mwanza Hotel (solo guitar), ili amwendeleze na akiwa pia mwana Bendi wetu. Alikuwa mwanafunzi mzuri alikuwa na bidii na akaweza baada ya muda mfupi kupiga programu yetu kubwa! Mimi nilikuwa mtunzi na mwimbaji licha ya kumiliki Ben…
Image
Orchestra Makassy katika moja ya awamu zake nyingi, baadhi ya wanamuziki hapa wapo jijini Dar es Salaam wakishughulika na mambo mbali mbali. Wakati huu Mzee Makassy alikuwa na vyombo vipya aina ya Ranger ambavyo vilipata umaarufu sana baada ya Franco na TP OK jazz kuja navyo katika ziara yao moja hapa Tanzania. Pichani ni Mzee Makassy anashughulika na kueneza injili na muziki wa injili. Mbombo wa Mbo mboka pia amefuata nyayo za Mzee Makassy na ni fundi maarufu wa vyombo vya muziki,Vivi, Malik,Kiniki Kieto,Seye Star,Ilunga,Shinga wa shinga,Tchimanga Assossa Kiongozi wa Bana Maquis, Okema, Marehemu Mzee Simaro (Aimala Mbutu) Baba mkwe wa Luiza Mbutu, Halfan Uvuruge, King Ray, Micky Jagger Jagger, Yusuph, Magoma Sony. Hapa ni enzi ya Jamani msinicheke kufilisika,

Wanamuziki wanawake

Image
Muziki wa dansi uliweza kupambwa na wanawake wengi waliopata sana umaarufu kutokana na umahiri wao enzi hizo. Wanamuziki wa dansi wanawake walichelewa sana kukubalika kwa wanamuziki wanaume tofauti na ilivyokuwa kwenye muziki wa aina nyingine kama taarab, na kwaya. Lakini wengi walijitokeza na kuzoa umaaruf mkubwa labda niwataje wachache na baadhi ya nyimbo zilizowapa umaarufu. Nianze na mama lao Tabia Mwanjelwa, huyu dada wa kinyakyusa alikuwa na sauti nzito ya kukwaruza lakini akiimba mwili utakusisimka. Pamoja na kuwa alikuwa akipanda katika majukwaa ya bendi mbalimbali ni bendi ya Maquis ndiyo iliyofanya hatua ya ziada na kumruhusu arekodi jambo ambalo lilikuwa gumu kwa wanawake katika bendi kabla ya hapo, wimbo uliompa umaaruf sana ni Jane..Jane mi nahangaika juu yako kwa maisha yako..... Pichani Tabia Mwanjelwa akiwa na gitaa, unaweza kupata mengineyo na kuwasiliana nae kupitia
Rahma Shally mwimbaji mwingine mahiri aliyepitia bendi nyingi na kurekodi kwanza na Mwenge Jazz…

Vijana Jazz Vs Maquis

Katika kipindi cha mwisho cha miaka ya 80, Kinondoni ilkuwa inawaka moto kwa Vijana siku ya Jumapili. Lang'ata ambayo baadae ilikuja kuwa Club ASET na sasa kanisa, palikuwa ndo ukumbi wa Dansi za kuanzia mchana kwa Bendi ya Maquis. Ukija hapa mbele Vijana Jazz Pambamoto awamu ya pili chini ya uongozi wa Hemed Maneti walikuwa nao kila Jumapili mchana wanaporomosha Dansi, na siku hiyo ilipewa jina Vijana Day. Kwa kweli Maquis walikuwa wanajaa watu na Vijana wanajaa watu. Kulikuweko na wapenzi wa kudumu wa Vijana kama ilivyokuwa Maquis. Wakati huo nyimbo kama Ngalula, Makumbele zilikuwa zinalia Lang'ata huku Vijana wanateremsha Shingo feni, Ngapulila, Azda. Ushindani huu ulilazimisha bendi kujitahidi kupiga vizuri na kwa displine au la wapenzi wanahamia bendi jirani. Kuna wakati Vijana Jazz walikuwa wanaanza muziki saa kumi na moja jioni na kupumzika saa tatu na nusu usiku kisha kumaliza dansi saa nne. Maquis wakawa wanaanza saa kumi na kumaliza saa tano usiku. Na wakaanza kuruhu…
Image
Kati ya Bendi ambazo Mzee J Mwendapole aliziendesha kwa muda mrefu ni Afriso ngoma. Hiyo ilikuwa bendi yake, ikawa na wanamuziki kama Maida na Belly Kankonde, iliweza kurekodi nyimbo kadhaa, lakini bendi hii iliongezeka umaarufu alipoingia marehemu Lovy Longomba, wakati huo akiwa na akina Kinguti system, Anania Ngoliga, Toffy Mvambe, Salim Shaaban Malik Nduka Masengo(Maliky Star) hao wakiwa waimbaji, Solo Gitaa- John Maida, Peter Kazadi, Robert Tumaini Mabrish, Rythm- Mjusi Shemboza, Bass-George na Kasongo, Drum -Ayub Karume, Abdul, Tumba- Magoma Sony, Trumpet-Juma Urungu, Ramadhani, Mbaraka Othman. wengi kati niliowataja wametangulia mbele ya haki. Baada ya hapo aliwahi pia kuwa na bendi ambayo ilikuwa na wanamuziki kadhaa kutoka sikinde ikawa inaitwa Sikinde Academia, ambayo haikudumu sana. Baada ya hapo amekuwa msaada mkubwa wa kuwasaidia wanamuziki wengi vyombo wakati wananzisha bendi zao.
Pichani ni Marehemu Lovy Longomba

Kwa heri Juma Mwendapole

Kwa masikitiko makubwa nimepata taarifa ya kifo cha mdau muhimu wa muziki wa dansi Juma Mwendapole. Amefariki Ijumaa tarehe 12 February 2010 na kuzikwa kesho yake. Mwendapole ndiye aliyekuwa mmiliki wa Bendi ya Afriso Ngoma iliyokuwa na wanamuziki maarufu kama Lovy Longomba. Kwa miaka ya karibuni wanamuziki wengi wamekuwa wakimtegemea kwa kukodi vyombo vya muziki toka kwake. Bendi nyingi zisingekuweko kama si msaada wa Juma Mwendapole.
Mungu Amlaze pema peponi Amin

Historia za mfumo wa Bendi

Utaratibu wa bendi hapa nchini ulifuata sana utaratibu wa bendi za nje kutokana na muziki wa bendi kuwa ni wa mapokeo. Hapa naongelea aina ya vyombo vilivyotumika stejini. Katika rekodi za kwanza zaidi za bendi kama vile zile za Cuban Marimba bendi zilipiga bila chombo chochote kilichotumia umeme kwa kuiga staili ya Cuba, na pia teknolojiaa ya vifaa vya umeme ilikuwa bado kuingia. Hivyo kulikuwa na gitaa moja na ngoma za kizungu (drums), bongoz, na vyombo vya kupuliza, filimbi, trumpet, saxaphone. Nyimbo za zamani za Salum Abdallah na Dar es Salaam Jazz Band zinatoa picha za vyombo hivyo. Mwanzoni mwa miaka ya 60, vifaa vya umeme vilianza kutumika na bendi kwa kawaida zilikuwa na Gitaa la bezi, rithim na solo,tarumbeta na saksafon. Halafu kulikuwa na bongoz. Baadae tumba zilichukua nafasi ya bongoz. Baadae bendi ziliingiza gitaa jingine ambalo liliitwa second solo. Hili lilikuwa gitaa ambalo lilipigwa katikati ya rithm na solo. Cuban Marimba katika kipindi fulani cha Mzee Kilaza aliw…
Image
Mwaka 1982/83 Tchimanga Kalala Assossa alianzisha na kuongoza bendi iliyoweza kutia changa moto katika ulimwengu wa muziki wakati huo. Bendi hiyo iliitwa Orchestra Mambo Bado na mtindo wake wa Bomoa Tutajenga Kesho. Wanamuziki katika bendi hiyo walikuwa Tchimanga Assossa, Kiongozi na muimbaji, Kazembe wa Kazembe mpiga solo (pamoja na jina hilo alikuwa Msukuma), William Maselenge, rythm guitar, Huluka Uvuruge second solo guitar, Sadi Mnala drums, Mzee Albert Milonge second solo, Lucas Faustin muimbaji, John Kitime muimbaji na rythm guitar, George Mzee muimbaji, Athuman Cholilo muimbaji, Likisi Matola Bass na keyboards, Jenipher Ndesile muimbaji, selemani Nyanga Drums. Album ya kwanza ya bendi hii ilikuwa na nyimbo zilizotamba kama vile Kutokuelewana, Bomoa Tutajenga Kesho , hii ilipigwa marufuku. Picha ya Assossa iliyotoka kwenye tangazo la kwanza la bendi, hapa akiwa amevaa shati la ndege ambalo kwa siku hizo walikuwa wanavaa wajanja tu.

Hemed Maneti

Image
Hemed Maneti mwanamuziki muimbaji aliyetokea Cuban Marimba na kutua Vijana Jazz mpaka kifo chake. Wimbo wa mwisho aliyorekodi uliitwa Nelson Mandela uliyotungwa na John Kitime. Wimbo huo ulitungwa ili kupigwa radioni wakati Mzee Mandela alipokuwa anatembelea Tanzania mara baada ya kuachiwa toka gerezani. Hakupanda tena jukwaani baada ya kurekodi wimbo huo.

Muziki wa soul

Image
Kila zama na vitabu vyake ni msemo unaoeleza kuhusu mambo ambayo hutokea katika kipindi fulani. Kila wakati kuna kizazi kipya, jambo ambalo kila kiza kipya kilichopo hudhani wao ndo wa kwanza. Katika miaka ya sitini kulikuwa na kizazi kipya cha wakati huo na moja ya muziki uliopendwa na kupigwa na vijana wakati huo ni muziki aina ya soul. Vijana walivaa kama wanamuziki wa soul wa wakati huo, walipiga muziki wao na bendi zilijipa majina ya bendi za soul. Ntataja baadhi ya wanamuziki ambao walipendwa na vijana wakati huo, najua kizazi kipya wa enzi hizo watakuwa na mengi ya kusema.OTIS REDDINGalileta raha kwa vibao kama Mr Pitiful, Fa-fa-fa-fa ambao Papa Wemba aliuimba tena miaka michache iliyopita. Sitting on the dock of the Bay, Respect, na wimbo ambao kila bendi ya soul iliupiga Direct Me. Otis alifariki katika ajali ya ndege ya kukodi na wanamuziki wenzake wane wa kundi lake la Barkays
Wilson Pickett alizaliwa March 18 1941, na kufariki kwa ugonjwa wa moyo Alhamisi 19 January 20…

Wanamuziki kutoka Kongo

Image
Huwezi kuongea kuhusu muziki wa bendi Tanzania bila kutaja wanamuziki kutoka Kongo. Kuna sababu kadha wa kadha. Kwanza historia. 1945 kwa sababu za kipropaganda Wamarikani walianzisha kituo cha radio kikubwa katika mji unaoitwa sasa Kinshasa hii iliwezesha muziki wa Wakongo kusikika katika eneo kubwa la Afrika ya kati na mashariki, 1947 ndugu wawili wa Kigiriki walianzisha record company katika mji unaoitwa sasa Kinshasa na santuri za wanamuziki kama Wendo Kolosay na nyimbo kama Akili ya bibi sawasawa mtoto mdogo zilisambazwa chini ya label ya Ngoma na Loningisa na kusambaa sana nchini kwetu, mambo haya mawili yaliweza kuusambaza muziki wa Kikongo katika maeneo yaliyoizunguka na kufanya wanamuziki kuanza kuiga mipigo ya Wakongo. Vita ya wenyewe kwa wenyewe ilianzisha kuhama kwa wanamuziki kutoka Kongo na kuja Afrika Mashariki. Kati ya wanamuziki wa kwanza kuja huku ni Paschal Onema. Lakini baada ya hapo zilikuja Bendi nyingi. Nakumbuka Super Bocca na wimbo wao Suzana mwana Tanzanie,…

Enzi za Buggy

Katika miaka ya 60 hadi katikati ya 70 kulikuwa na bendi nyingi za vijana ambazo unaweza kulinganisha na wanamuziki wa sasa wanaojulikana kama kizazi kipya. Katika jiji la Dar es Salaam, kulikuweko na bendi nyingi kama vile The Sparks, The Comets, The Flames, The Jets, Crimson Rage, The Lovebugs, Trippers Imagination, Safari Trippers, Afro 70. je unakumbuka nyingine ?

Bendi Zetu

Tanzania tuna bahati mbaya ya kutokuweka kumbukumbu nyingi sana. Kati ya hizo ni kumbukumbu za bendi gani au vikundi gani vya muziki viliwahi kuweko. Labda tusaidiane kila mmoja wetu ajaribu kukumbuka ni kikundi gani kilikuweko wilayani kwake nianzae na mifano michache
******
Iringa-
Highland Stars
Tancut Almasi Orchestra
Chikwala chikwala
Ruaha International
Vico Stars
Mkwawa Orchestra
******

Morogoro
La Paloma Jazz
Cuban Marimba
Morogoro Jazz
Les Cubano
Vina vina Orchestra
******

Ifakara
Sukari Jazz
Kilombelo Jazz
Malinyi Jazz
Kwiro Jazz
Mahenge Jazz
******

Tanga
New Star Jazz
Jamuhuri Jazz
Atomic Jazz
Tanga International
Amboni Jazz
******

Tabora
Tabora Jazz
Nyanyembe Jazz
Kiko Kids haya tuendelee
******

Mwanza
Orchestra Super Veya
******

Moshi
Orchestra Zaire Success
Bana Africa Kituli
********

Mpwapwa
Mpwapwa Jazz
******

Dodoma Jazz
Dodoma International
Materu Stars
Saki Band
Super Melody
*****

Songea
Tembo Jazz
Orchestra Sere sere
******

Lindi
Mitonga Jazz
******

Masasi
Kochoko Jazz

Mzee Humplick aliwahi kupigwa marufuku

Je unajua kuwa Mzee Frank Humplick ambaye ndiye mtunzi wa nyimbo kama Chaupele Mpenzi, Embe dodo imelala mchangani, aliwahi kutunga nyimbo iliyopigwa marufuku na kusakwa nyumba hadi nyumba ili kusibakie hata nakala ya wimbo huo? Maneno ya wimbo huo yalisema hivi:
Uganda nayo iende Tanganyika ikichangaruka, Kenya na Nyasa zitaumana Nasikia fununu wanavyoichanachana China, Kitisho! I am a democrat, I don't want communism, English, Yes, No I don't know, Kizungu sikijui Wanyika msishindane na Watanganyika Wimbo huo ukaanza kutumika kabla ya mikutano ya Mwalimu Nyerere na kuanza kuwa maarufu kama wimbo wa kudai uhuru, wakoloni haraka sana wakaona wimbo huu utaweza kusababisha vurugu kama ambazo zilikuwa zinaendelea Kenya chini ya Maumau. Serikali ikaupiga marufuku na kuanza kuusaka nyumba hadi nyumba
Young Audiences Music Award

2 February 2010, Jeunesses Musicales International (JMI) launches a call for nominations for the Young Audiences Music Award 2010, an international prize that will celebrate top musical productions for children and youth. "Looking at the quality of productions presented in schools and within education and audience development programs today, it's obvious that a new standard has been set" said JMI Secretary General Blasko Smilevski "What we see are productions nothing short of spectacular - in terms of artistry but also in terms of message. The once common ‘What instrument is this? lesson' is being fast replaced by subtle teachings on social, environmental, and intercultural issues through music."Do you know a young audiences production with impact? Visit the all-new www.yama-award.com to apply today! Deadline for submissions is May 1st 2010, thereafter an international panel of experts will select 5 finalists to be presented onli…
Image
Mara nyingine mtu unaweza kuanza kupata picha kama vile wanamuziki wako Dar es Salaam tu, jambo ambalo si kweli. Japo ukweli ni kuwa zamani kulikuweko na Bendi karibu kila wilaya nchini. Hapa ni bendi 2 kutoka Dodoma. Super Melody na Saki Stars.
Mwenye gitaa na jaketi la rangi mbili ni Mzee Ikunji, huyu pamoja na kupigia bendi kama Tabora Jazz pia alikuweko Tancut Almasi Orchestra na ndie aliyepiga second solo kwenye nyimbo kama Masafa Marefu, Nimemkaribisha nyoka, na Kashasha

Image
Hii ni Bendi inayoitwa Karafuu Band,moja ya bendi kadha wa kadha zilizo na masikani Zanzibar. Mwenye miwani ya jua ndio kiongozi wa bendi anaitwa Anania Ngoliga, ni mwanamuziki mwenye ulemavu wa macho lakini kati ya wanamuziki mahiri Tanzania. Anania ambaye kwa wakati huu yuko Marekani katika tour ambayo anasindikizana na mwanamuziki Bela Fleck. Fleck amepata grammy awards 3 mwaka huu. Na katika album iliyopata awards kuna nyimbo 2 ambazo zimetungwa na Anania. Anania kisha kuwa mwanamuziki katika bendi ya Legho Stars, Afrisongoma, Tango Stars, Tacosode Band. Amesharekodi na wanamuziki wengi mahiri wakimataifa akiwemo Kriss Kristoffeson, na Zapmama

Image
Hapa kuna wakubwa wawili katika ulimwengu wa soka, Sylersaid Mziray, kocha anaeheshimika sana, na Mzee Hassan Dalali mwenyekiti wa Simba Sports Club enzi hizo akiwa Kiongozi na mpigaji solo wa bendi ya Vijana Jazz.Mziray alikuwa katembelea Kilimanjaro Band wananjenje.
Image
Kati ya mwanamuziki Mtanzania ambae historia hajamtendewa haki kutokana na kutothaminiwa kwa kazi zake ni marehemu Mzee Frank Humprik. Mzee Humprik anaeonekana hapa katika picha ya rangi ameishi kwa miaka mingi ya mwisho wa maisha yake Lushoto. Mzee huyu akiwa na dada zake wawili walitikisa anga za muziki wa Afrika ya Mashariki, na bado wanaendelea kufanya hivyo japo hawatambuliwi kabisa. Kundi lao lililoitwa Frank na dada zake waliuletea ulimwengu nyimbo kama Embe dodo imelala mchangani, Kolokolola, Chaupele Mpenzi na nyingine nyingi ambazo bendi bado zinapiga nyimbo hizo mpaka leo na baadhi ya wanamuziki wamekuwa wanazirekodi bila hata kutaja mtunzi wa nyimbo hizo. Mbaya zaidi mara nyingi nyimbo hizo zimekuwa zikitambulishwa kama nyimbo za mwanamuziki mwingine kutoka Kenya marehemu Fundi Konde.
Mzee Fundi Konde ambae hapa chini yuko na mwanamuziki mwingine maarufu wa Kenya Fadhili William aliyeimba Malaika, ndiye aliyetuachia nyimbo kama Ajali haikingi, Mama Leli, Wekundu si hoja…

Mzee Frank Humprick

Image
Kati ya mwanamuziki ambae hajatendewa haki kutokana na kutothaminiwa kwa kazi zake ni marehemu Mzee Frank Humprick. Mzee huyu akiwa na dada zake walitunga nyimbo nyingi sana ambazo mpaka leo zinapigwa majukwaani na karibu kila bendi Afrika mashariki. Bendi nyingine zimediriki kurekodi upya nyimbo hizo tena bila hata kumtaarifu Mzee huyu au nduguze. Baya zaidi ni nyimbo zake nyingi kutambulishwa kuwa ni za Fundi Konde. Nyimbo zake kama Embe dodo imelala mchangani, Chaupele mpenzi,I am a democrat(uliopigwa marufuku wakati wa mkoloni),Kolokolola na nyingine nyingi. Mzee huyu Mtanzania aliyekuwa akiishi Lushoto mpaka kifo chake anastahili kuenziwa na wapenzi wote wa muziki Tanzania.
Image
John Mwenda Bosco,ni kati ya wanamuziki ambao w alileta mabadiliko mengi katika muziki wa Afrika ya Mashariki. Muziki wake unapendwa sana mpaka leo. Je unajua alikuwa nani? Peter Colmore ambaye alifanya kazi kwa karibu sana na Mzee Ally Sykes ambaye kwa bahati mbaya hajatunukiwa nafasi anayostahili katika historia ya muziki wa Tanzania ndie aliye mleta John Mwenda Bosco Afrika ya Mashariki. Bosco alitambulishwa kwa Colmore kupitia Edward Masengo,mwanamuziki mwingine toka Kongo ambae alikuwa maarufu sana na hasa kutokana na matangazo ya biashara yaliyokuwa yanafanywa na kampuni ya Colmore na Mzee Sykes, Colmore akalazimika kumfuata Bosco hadi Congo ambapo serikali ya Kibergiji wakati huo ilimlazimisha alipe Faranga 30,000 kama pesa ya kuhakikisha atamrudisha Bosco kwao. Bosco alikuwa tayari anajulikana sana Afrika ya Mashariki kupitia santuri zake. Kati ya nyimbo maarufu za Bosco ni ule wimbo wa ala tupu ambao hutumika na Radio Tanzania kuashiria kuanza kwa kipindi cha zilipendwa.
Image
Taarab
Muziki wa Taarab unautata wa vyanzo viwili. Kuna wanaosema taarab iliingia nchini mwetu kupitia ikitokea Mombasa. Kuna tafiti nyingine ambazo zinaonyesha Sultan Barghash wa Zanzibar aliwapeleka wanamuzikiwawili Misri kujifunza upigaji wa Taarab,na hao waliporudi ndo walipanda mbegu ya Taarab nchini mwetu. Taarab imekuwa nahistoria ambayo ya kuwa na aina nyingi za taarab, na mpaka leo mabadiliko ya taarab yanaendelea. Imefikia sasa kuna hata vikundi vya taarab vina wacheza show. Taarab imekuwa pia ni ya kucheza na si kusikiliza ujumbe tu kama ilivyokuwa zamani
Image
Extra Bongo ya Ally Choky kazini


Image
Vijana Jazz Band wakisubiri kupiga muziki katika siku ya kumpokea Mzee Nelson Mandela mara baada ya kuachiwa kifungoni, hapa wakiwa stadium Morogoro. Toka kushoto waliosimama John Kitime kwa sasa yupo Kilimanjaro Band, Marehemu Agrey Ndumbalo, Mhasibu wa Bendi, Abou Semhando yupo African Stars (Twanga Pepeta),Marehemu Fred Benjamin, Said Mnyupe yuko Msondo,Said Mohamed Ndula, Rashid Pembe anendelea na muziki Mak Band, Hassan Show yupo Malasyia na Kinguti System wakipiga muziki huko. Waliokaa mpenzi wa bendi, marehemu Bakari Semhando, Juma Choka yupo sikinde.

Picha ya chini, Mohammed Gotagota, Freddy Benjamin,Mhando,Said Mohamed 'Ndula',Rashid Pembe,Aggrey Ndumbalo, hiyo ndo Vijana Jazz Saga Rhumba
Image
Tancut Almasi Orchestra, bendi iliyokuwa namakazi yake Iringa kuanzia 1987, ilikuwa chini ya Kiwanda cha kuchonga almasi cha hapo Iringa, Diamond Cutting Company. Bahati mbaya wengi ni marehemu. Kutoka kushoto Buhero Bakari inasemekana ni mganga wa dawa za asili kwa sasa,marehemu Kyanga Songa, Kasaloo Kyanga yupo Dar anaendelea na muziki,Kabeya Badu, yuko na King Kiki na wazee sugu, Marehemu Kalala Mbwebwe, Abdul Mngatwa, yuko Iringa ameacha muziki, Akuliake Salehe aka King Maluu yupo Dar anaendelea na muziki
Image
Image
UMUHIMUWA KULIPIA MATUMIZI YA MUZIKIUkitunga wimbo na ukiiweka katika hali ya kushikika marahiyo unaanza kupata haki zote za wimbo hiyo. Wimbo ni mali itokananyo na ubunifu hivyo moja kwa moja unapata haki zinazostahili kutokana na mali hiyo na ni mali yako kama vile mali nyingine. Mara wimbo utakapokuwa tayari kutumika ni muhimu kusajili katika sehemu husika ili uweze kupata ulinzi na stahili zitakazopatikana kutokana na mali hiyo. Kuna haki za aina mbili, Performance Rights na Mechanical Rights.Performance Rights ni zile haki zitokanazo na tungo ya muziki kutumika hadharani au kurushwa hewani. Hii inajumlisha pamoja na muziki kupigwa na Live Band na, au hata muziki uliokwisha rekodiwa kupigwa hadharani katika sehemu za hadhara kama restaurants, bar, klabu za usiku, kwenye maharusi, na kadhalika. Performance rights pia ni haki zinazoambatisha muziki kurushwa hewani kupitia radio na televisheni. Kutokana na kuweko kwa haki hizi, watu binafsi na makampuni ambayo yangependa kutumia kazi…